'Ujauzito wangu na Diamond uliharibika,' Official Lyn azungumza kuhusu mahusiano yake na Diamond Platnumz

Muhtasari

• Lyn alisema mahusiano yake na Diamond yalidumu kwa kipindi  cha mwaka mmoja unusu.

•Lyn alisema alikuwa na matumaini makubwa ya kufunga ndoa na Diamond kwani tayari alikuwa amepiga hatua ya kuenda nyumbani kwao kujitambulisha kwa wazazi.

•Mwanasoshalaiti huyo alidai katika kipindi ambacho alikuwa anachumbia Diamond alipata ujauzito ila ukaharibika kwa sababu ambazo hakuzifahamu.

Diamond na Official Lyn
Diamond na Official Lyn
Image: HISANI

Mwanasoshalati na mwanamuziki kutoka Tanzania Irene Louis almaarufu kama Official Lyn amefunguka kuhusu mahusiano yake na nyota wa bongo Diamond Platnumz.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Wasafi Media siku ya Jumatatu, Lyn alisema mahusiano yake na Diamond yalidumu kwa kipindi  cha mwaka mmoja unusu.

Mwanasoshalaiti huyo alifichua kuwa walipatana na Diamond kwa mara ya kwanza katika kipindi cha kurekodi video ya wimbo wa Rayvanny.

"Tulikutana siku ambayo nilienda kukutana na Rayvanny kurekodi video. Tulienda na Darleen kwenye saluni tukatengezwa. Keshoye asubuhi tukakutana kwenye sehemu tukaenda kushoot ndio tukajuana" Lyn alisema.

Lyn alisema alikuwa na matumaini makubwa ya kufunga ndoa na Diamond kwani tayari alikuwa amepiga hatua ya kuenda nyumbani kwao kujitambulisha kwa wazazi.

"Diamond alikuja hadi nyumbani kwetu. Naweza sema mimi ni tofauti kuliko wale wengine. Alikuja kujitambulisha na  kuleta barua ya posa kwamba tulikuwa na yeye na amenipangia. Watu wake walikuja nyumbani" Alisema Lyn. 

Mwanasoshalaiti huyo alidai katika kipindi ambacho alikuwa anachumbia Diamond alipata ujauzito ila ukaharibika kwa sababu ambazo hakuzifahamu.

Lyn alisema moyo wake uliumia sana wakati alipoteza ujauzito wake.

"Tayari nilikuwa na ujauzito ambao uliharibika. Ulikuwa wa Diamond. Uliharibika baada ya miezi mitatu" Lyn alisema.

Lyn na Diamond wanaaminika kuchumbiana mwaka wa 2018 .