•Konde Boy aliweka wazi kwamba hana chuki yoyote dhidi ya wanawake wa Bongo huku akieleza kuwa kabla ya kufanya maamuzi ya kuchumbia mwanadada kutoka nje ya mipaka ya nchi yake alifanya majarabio kadhaa na wanawake wa kitanzania ila hakuwahi kuwa na imani moyoni.
Hivi majuzi mwanamuziki wa Bongoflava Rajab Abdul Kahali almaarufu kama Harmonize ametambulisha kipenzi chake kipya hadharani baada ya kutokuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha takriban nusu mwaka.
Harmonize alimtangaza Briana kama malkia mpya kwenye ufalme wake huku akiahidi kumpenda na kumlinda siku zote za maisha yake.
Alipokuwa anahutubia wanahabari siku ya Alhamisi punde tu baada ya kutua Tanzania kutoka Marekani, Harmonize alieleza sababu zake kujitosa kwenye mahusiano na mwanadada huyo mrembo kweli mwenye asili ya Australia.
Konde Boy aliweka wazi kwamba hana chuki yoyote dhidi ya wanawake wa Bongo huku akieleza kuwa kabla ya kufanya maamuzi ya kuchumbia mwanadada kutoka nje ya mipaka ya nchi yake alifanya majarabio kadhaa na wanawake wa kitanzania ila hakuwahi kuwa na imani moyoni.
"Hapa Tanzania kuna wanawake wengi hata kuliko Briana. Lakini imefika mahali hata mwanamke wa hapa Tanzania namuogopa. Namwogopa naona anaweza kutumika. Naona naweza ingia kwenye mahusiano naye kisha akatumika. Wanaweza wakamfanya kama walivyofanya na mtu mwingine. Nilihangaika huku na huku na mwenyezi Mungu akaniletea Briana" Harmonize alisema
Staa huyo wa Bongo alimshtumu bosi wake wa zamani Diamond Platnumz kwa kuvunja mahusiano yake mawili ya awali na kumkosanisha na Rayvanny.
Harmonize alidai Diamond ndiye aliyepanga njama za kuharibu mahusiano yake na Sarah Michelloti pamoja na ya hivi karibuni na mwigizaji Fridah Kajala.
"Naamini asilimia mia, yeye amehusika kuvunja hayo mahusiano. Na hata suala la kuvunjisha video yangu ya uchi, alikuwa anataka kupiga ndege watatu kwa jiwe moja. Kama mtu mwenye akili timamu asingeruhusu Rayvanny kama msanii wake achapishe video yangu ya utupu. Ni kweli iliniharibia sawa, lakini pia yeye ilimharibia. Alijua mimi nitalipiza kisasi. Alijua ningemlipizia Rayvanny. Ina maana alitaka kuua ndege wawili. Alijua nilikuwa kwenye mahusiano na Kajala na siwezi kosa video ya uchi ya Kajala. Alijua nikipanic nitavunjisha video ya Kajala" Harmonize alisema.
Harmonize alisema Diamond alitumia mwanadada mcheza densi wa Wasafi ambaye alikuwa rafiki wa mpenzi wake Sarah Michelloti kuvunja ndoa yao ya miaka minne.
Alidai Diamond alivunja mahusiano yake na Sarah ili kumwangusha kwa kuwa aliamini kwamba Muitaliano huyo ndiye alikuwa anamsaidia kifedha.