logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mtozeni ushuru na muache aweke pesa zake!" Huddah Monroe atetea mwanadada aliyetumiwa milioni 102 na mpenziwe Mbelgiji

Huddah amefichua kwamba alipokuwa na umri wa miaka 21 mpenzi wake alimnunulia gari yenye thamani ya milioni 7.5.

image
na Radio Jambo

Habari20 November 2021 - 10:37

Muhtasari


•Felista Nyamathira Njoroge 21,  amekuwa akivuma sana mitandaoni hivi karibuni baada ya kudai kuwa mpenzi wake Mbelgiji De Mesel Marc, alimtumia pesa hizo kama zawadi.

•Huddah amefichua kwamba alipokuwa na umri wa miaka 21 mpenzi wake alimnunulia gari yenye thamani ya milioni 7.5.

•Huddah amesema Assets Recovery imeshangazwa na wingi wa pesa zilizo kwenye akaunti ya Felista kwa kuwa hawajazoea kuona wanaume wanaotumia wapenzi wao pesa nyingi kama zile

Mwanasoshalaiti Huddah Monroe  amejitokeza kutetea mwanafunzi wa chuo cha kiufundi cha Nairobi anayedaiwa kuwindwa na Shirika la Assets Recovery baada ya shilingi milioni 102 kupatikana zikiwa zimehifadhiwa kwa akaunti yake ya benki.

Felista Nyamathira Njoroge 21,  amekuwa akivuma sana mitandaoni hivi karibuni baada ya kudai kuwa mpenzi wake Mbelgiji De Mesel Marc, alimtumia pesa hizo kama zawadi

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Huddah amedai ni kweli kuna wanaume ambao huwatuza wapenzi wao kwa pesa nyingi au zawadi za thamani kubwa kama ishara ya mapenzi..

Huddah amefichua kwamba alipokuwa na umri wa miaka 21 mpenzi wake alimnunulia gari yenye thamani ya milioni 7.5.

Pia alidai alipokuwa na umri wa  miaka 19 hivi mpenzi wake angemtumia pesa nyingi mara kwa mara, jambo ambalo lilifanya afungiwe akaunti yake mara nyingi.

"Hii yaweza kuwa kweli. Zawadi kutoka kwa mpenzi. Benki ya Co-op ilinifungia akaunti yangu mara nyingi nikiwa na miaka 19 hivi. Sababu mpenzi wangu alininunulia gari ya kwanza nikiwa na umir wa miaka 21 (Ilikuwa dola 75,000 hivi, hizo ni shilingi milioni 7.5 za Kenya kwa wakati ule)  hatukutumia akaunti yangu.Hiyo ingeibua maswali mengi. Wanaume wajanja wanajua kufanya mambo" Huddah amesema.

Huddah amesema Assets Recovery imeshangazwa na wingi wa pesa zilizo kwenye akaunti ya Felista kwa kuwa hawajazoea kuona wanaume wanaotumia wapenzi wao pesa nyingi kama zile.

Kulingana na Huddah, mamilioni ambayo mpenzi wa Felista alimtumia ni pesa za ziada tu kwake kwa kuwa yeye ni bwenyenye mkubwa.

"Wanaume wanapatiana pesa mingi huko nje kama pesa za mfukoni. Wengine wao, sio wote. Lakini watu wa Assets wamezoea wababa wa Kenya. Wao hupatiana pesa za mfuko kweli? Hizo milioni 110 huenda ni pesa za ziada tu, kuona kwamba jamaa huyo anajishughulisha na Crypto currency na mambo mazuri. Mkate ushuru na mmwache aweke pesa zake!" Huddah amesema.

Assets Recovery wanadaiwa kumfuata Felista wakimhusisha na biashara ya 'Wash Wash' inayohusisha raia wa kigeni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved