"Bro kwani unanitaka, mimi sio wa chama hicho!" Willy Paul atahadharisha Eric Omondi amkome

Muhtasari

Kwa kipindi cha siku kadhaa ambazo zimepita wasanii hao wawili wasio wageni kwenye drama wamekuwa wakitupiana vijembe katika mtandao wa Instagram.

•Willy Paul alimkea vikali mchekeshaji huyo akidai kuwa umaarufu wake uliisha kitambo na vichekesho vyake viliisha ladha.

•Willy Paul ameonekana kughadhabishwa na mazoea ya  mchekeshaji huyo kuendelea kumkejeli huku akimwagiza akome kabisa.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL, ERIC OMONDI

Ugomvi kati ya mwanamuziki Willy Paul na mchekeshaji Eric Omondi mitandaoni hauna dalili za kuisha hivi karibuni.

Kwa kipindi cha siku kadhaa ambazo zimepita wasanii hao wawili wasio wageni kwenye drama wamekuwa wakitupiana vijembe katika mtandao wa Instagram.

Ugomvi ulianza rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Willy Paul kutambulisha msanii mpya wa kike aliyesajili katika lebo yake ya Saldido, Queen P.

Baada ya kumtambulisha, Willy Paul aliendelea kushirikiana na  Queen P waliendelea kwa wimbo 'Pressure' ambao ulichapishwa YouTube siku ya Jumamosi, jambo ambalo halikumpendeza kabisa Eric Omondi ambaye alimshtumu kwa kukosa uhalisi na ubunifu.

"Ngoma kali sanaa lakini kitu tu umekosa ni ORIGINALITY Bro, CREATIVITY pia iko chini Kiasi lakini jitihada iko👍👍👍. Alafu vile kutakuwa na Willy Paul mmoja tu, kunaweza kuwa ONE 'P'. Badilisha jina la Msanii Buda. Lakini kazi poa" Omondi alimwambia Willy Paul.

Willy Paul alimkea vikali mchekeshaji huyo akidai kuwa umaarufu wake uliisha kitambo na vichekesho vyake viliisha ladha.

Paul alimkosoa Omondi kwa kutofurahia kitendo chake cha kusajili mwanamuziki mgeni wa kike huku akidai amepoteza heshima yote aliyokuwa nayo kwake.

Je, Ni mbaya kusaidia watu katika nchi hii? Hivi sasa nimesaini msanii mpya wa kike na kutoa wimbo 'Pressure'' Naye huyu wazimu anapenda kupanda watoto ananitukana?? @ericomondi naomba uniache.. Nimepoteza heshima yote niliyokuwa nayo kwa mwili wako mkonde. Tafadhali endelea kuvaa kama mwanamke kwa amani" Willy Paul alimwambia Eric Omondi.

Licha ya hayo Omondi aliendelea kumtupia Willy Paul vijembe huku akiampa kupambana naye hadi atakapokubali kuenda kanisani kutumbu dhambi zake na arejelee kuimba ngoma za injili.

Willy Paul ameonekana kughadhabishwa na mazoea ya  mchekeshaji huyo kuendelea kumkejeli huku akimwagiza akome kabisa.

"Bro kwani unanitaka? Umenitufuta sana... mimi sio wa hio chama! Acha kutaja jina langu kila mahali .Nadhani wimbo wangu umekusimamishia damu sindio? Wewe kana watu wako uko. #shinikizo kwa dunia. Tafuta bibi uoe!"  Willy Paul amemwambia Omondi.