Diamond Platnumz anamiliki nyumba na viwanja 67 Tanzania- Mpenzi wa mamake afichua

Muhtasari

•Shamte ambaye amekabidhiwa majukumu ya kusimamia miradi  ya nyumba za Diamond alisema kufikia sasa mwanamuziki huyo amefanikiwa kununua viwanja 67 na kujenga nyumba katika kila kiwanja.

•Aliweka wazi kwamba nyumba hizo 67 za  nyota huyo wa muziki anayeshabikiwa sana kote bara Afrika ni za kupangisha wala sio zake mwenyewe kukaa.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM

Thamani  ya jumla ya mwanamuziki mashuhuri kutoka TanzaniaNaseeb Abdul Juma almaarufu kama Diamond Platnumz imeendelea kwa kasi mno katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.

Aghalabu staa huyo wa bongoflava ameonekana akajigamba na mali yenye thamani kubwa ikiwemo magari, nyumba , mavazi na mapambo ya thamani.

Uncle Shamte ambaye ni mpenzi wa mamake Diamond, Mama Dangote amefichua kuwa Diamond amefanikiwa kujenga makumi ya nyumbi katika maeneo mbalimbali Tanzania.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Wasafi Media,Shamte ambaye amekabidhiwa majukumu ya kusimamia miradi  ya nyumba za Diamond alisema kufikia sasa mwanamuziki huyo amefanikiwa kununua viwanja 67 na kujenga nyumba katika kila kiwanja.

"Naseeb ana nyumba nyingi. Nyumba kama 67 . Mimi binafsi nina miaka  mitano kwenye familia, sasa nasimamia nyumba ya 61. Hatujipi sifa kusimamia nyumba lakini tunapozungumza sasa hivi hivyo ndivyo uwezo wake ulivyo" Alisema Uncle Shamte.

Aliweka wazi kwamba nyumba hizo 67 za  nyota huyo wa muziki anayeshabikiwa sana kote bara Afrika ni za kupangisha wala sio zake  mwenyewe kukaa.

Shamte ambaye amekuwa kwa familia ya kina Diamond kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita amesisitiza hatua ya mwanamuziki huyo kujenga nyumba nyingi haimaanishi kwamba anashindana na yeyote kwa utajiiri.

"Sio nyumba za kuishi. Ni nyumba za kupangisha. Ana nyumba na viwanja 67. Sio kushinda, huenda zikawa nyingi ama kidogo lakini huo ndio uwezo wake kajikuna kafikia hapo" Alisema Shamte.

Vilevile alipuuzilia mbali madai kuwa ndoa yake na mamake Diamond imevunjika baada ya uvumi kutanda kote Bongo kwamba kitumbua kimeingia mchanga .

Shamte aliweka wazi kuwa wangali pamoja na hamna msukosuko wowote katika ndoa yao ya miaka mitano.

"Kuachana iweje. Sisi wenyewe ni Waislamu na kwetu talaka ni dhambi. Sio kitu kizuri. Sio kitu cha kushabikia wala kuongelea ama kushauri mtu ampe  mwenzake talaka. Sisi hatuko huko" Uncle Shamte alisema.