"Meet my daughter!" Kabi hatimaye amkaribisha binti yake Abby kwa familia ya Wajesus ya mitandaoni

Muhtasari

•Kabi ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na wimbo wake 'Bonoko' alisema aliridhika sana kupata muda wa kufarahia pamoja na binti yake huku akidai anatazamia kupata nafasi kama ile tena na tena.

•Milly alimkaribisha Abby vizuri na kwa upendo mwingi huku akisema  anajivunia mumewe na binti huyo ambaye alipata na mwanadada mwingine takriban miaka minane iliyopita.

•Mapema mwaka huu Kabi alishambuliwa sana mitandaoni baada ya kukiri kuwa ndiye baba mzazi wa Abby ingawa hapo awali alikuwa amekana madai hayo.

Kabi Wajesus na Milly Wajesus
Kabi Wajesus na Milly Wajesus
Image: INSTAGRMA// KABI WAJESUS

Hatimaye mwanavlogu na mfanyiashara Peter Kabi almaarufu kama Kabi wajesus amekaribisha binti yake Abby kwenye familia yake ya mitandaoni, 'The Wajesus Family' 

Kupitia ujumbe ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Kabi alisema ana furaha kubwa kuona bintiye akijiunga na familia ya Wajesus ya mitandaoni.

Kabi pia alimfungulia binti yake ukurasa wa Instagram @abbywakabiwajesus ambao tayari umesajili zaidi ya wafuasi elfu nane masaa machache tu baada ya kuzinduliwa.

"Nimefurahia sana kuwa binti yangu Abby hatimaye anajiunga na familia yetu ya mtandaoni" Kabi aliandika kwenye ukurasa wake wa instagram na kuambatinisha ujumbe wake na picha yake akiwa pamoja na Abby.

Kwenye video ambayo alipakiwa katika chaneli ya YouTube ya 'The Wajesus Family', Kabi na Abby  walionekana wakijiburudisha pamoja katika date yao ya kwanza.

Kabi ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na wimbo wake 'Bonoko' alisema aliridhika sana kupata muda wa kufarahia pamoja na binti yake huku akidai anatazamia kupata nafasi kama ile tena na tena.

"Binti yangu @abbywakabiwajesus. Ilikuwa siku nzuri zaidi maishani mwangu. Natazamia haya na zaidi" Kabi alisema.

So happy my daughter Abby gets to join our online family.

 

Mke wa Kabi, Milly Wajesus alionekana kufurahia sana hatua ya Abby kujiunga na familia yao ya mitandaoni huku akiwasherehekea wawili hao.

Milly alimkaribisha Abby vizuri na kwa upendo mwingi huku akisema  anajivunia mumewe na binti huyo ambaye alipata na mwanadada mwingine takriban miaka minane iliyopita.

"Karibu kwa familia yetu ya mitandaoni baby girl. Tunakupenda @abbywakabiwajesus. Najivunia nyinyi wawili. Wakati wa Mungu ndio mzuri zaidi" Alisema Milly.

Milly alipakia picha ya wawili hao na kusema wanapendeza sana.

Mapema mwaka huu Kabi alishambuliwa sana mitandaoni baada ya kukiri kuwa ndiye baba mzazi wa Abby ingawa hapo awali alikuwa amekana madai hayo.

Baada ya vipimo vya DNA kufanyika ilibainika kwa kweli kuwa binti huyo mwenye umri wa miaka 8 ni wa Kabi.

"Ningetaka kudhibitisha kuwa matokeo ya DNA yalitolewa na kubaini kuwa mimi ndiye baba mzazi wa mtoto. Matokeo yanathibitisha kuwa, mnamo 2013 (ambayo ilikuwa kabla ya kuokoka na kuoa), nilimpata Abby"Kabi alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram mnamo mwezi Mei 2021.

Baadhi ya wanamitandao walitumia nafasi hiyo kumshambulia Kabi haswa kwa kuwa hapo awali alikuwa amekana kuwa ndiye baba huku akieleza kuwa mama ya Abby anayefahamika kama Shiko ni binamu yake.