Ndoa inapaswa kuheshimiwa,sio uhusiano wa kawaida -Anerlisa Muigai

Muhtasari
  • Anerlisa Muigai amemkashifu aliyekuwa mume wake Ben Pol kwa kutoheshimu ndoa yao

Anerlisa Muigai amemkashifu aliyekuwa mume wake Ben Pol kwa kutoheshimu ndoa yao miezi chache baada ya wawili hao kuachana.

Akizungumza na waandishi wa habari wa  Tanzania, Anerlisa anasema aliumia baada ya Ben Pol kumwaga chai kuhusu ndoa yao.

"Kitu ambacho watu hawaelewi  na kufahamu ni kwamba ndoa si kama uhusiano mwingine wowote. Ndoa ni taasisi inayopaswa kuheshimiwa na hupaswi kuizungumzia ovyo," Alizungumza Anerlisa.

Anerlisa anasema chochote Ben Pol alifanya kinaenda kinyume na kile walichofundishwa baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha.

"Tulienda kwenye kikao cha mafunzo cha kanisa ambapo tulishauriwa kutozungumza kuhusu ndoa yetu kuhusu kile kitakachotokea baada ya hapo... Mkienda tofauti na iwe hivyo lakini kuzungumzia ilikuwa ni jambo kubwa sana," alisema.

Anerlisa alifichua kwamba mwimbaji huyo wa Tanzania alibadili dini na kuwa Muislamu kabla ya kurejea Ukristo baada ya wiki mbili.

Anerlisa anasema hatajutia kuchumbiana wala kuachana na Ben Pol kwa sababu anaamini kila kitu ni funzo.