"Msizunguke, kunywa au kulala na wadosi wenu!" Akothee awashauri mabinti wake baada ya kuhitimu chuo kikuu

Muhtasari

•Akothee aliwataja Vesha na Rue Baby kama kielelezo bora kwa wasichana wadogo huku akiwaagiza watumie ushawishi wao kuonyesha wasichana wengine mwelekeo mzuri wa maisha.

•Aliwashauri kuhusu jinsi ya kujibeba wakiwa kazini na watakavyohusiana na wadosi pamoja na wafanyakazi wenzao.

Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Image: Instagram

Alfajiri ya Jumatatu mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu kama Akothee aliraukia kuandikia mabinti wake Vesha Okello na Aggrey Dion Okello (Rue Baby) ujumbe wa pongezi na ushauri kufuatia hatua yao ya kukamilisha masomo ya chuo kikuu na kuhitimu.

Mwanamuziki huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mabinti wake kwa kurahisisha kazi yake kama mzazi.

Akothee aliwataja Vesha na Rue Baby kama kielelezo bora kwa wasichana wadogo huku akiwaagiza watumie ushawishi wao kuonyesha wasichana wengine mwelekeo mzuri wa maisha.

"Barua kwa wahitimu wangu wawili @veshashaillan na  @rue.baby. Asante sana kwa kuwaonyesha wasichana wadogo mwelekeo sahihi wa kuwa mtoto kwanza, mwanafunzi, hadi kuwa  watu wazima. Baadhi yetu hatuna kitu ambacho wazazi wetu wangeweza kusherehekea. Toka kuruka uzio kukimbiza mimba na kurudi kulaumu kila mtu.  Asante kwa kurahisisha kazi yangu kama mzazi @rue.baby @veshashaillan. Sasa nataka muende ulimwenguni na muelekeze wasichana wengi iwezekanavyo. Tembea kila wakati na kichwa chako juu. Nyinyi tayari ni wahitimu" Aliandika Akothee.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 41 aliwatahadharisha mabinti wake dhidi ya kutumia jina lake wanapotafuta ajira licha ya kuwa lina ushawishi mkubwa huku akiwaarifu kuwa huenda likawasababishia madhara.

Aliwashauri kuhusu jinsi ya kujibeba wakiwa kazini na watakavyohusiana na wadosi pamoja na wafanyakazi wenzao.

  • Muwe wanyenyekevu kama kawaida.
  • Shahada ni nadharia, sasa pateni uzoefu na muwe na kazi maadili kazini. Vitendo huleta matokeo
  • Kuwa na ufahamu wa wakati, humna mengi yaliyobaki.
  • Epuka roho ya kuahirisha mambo,huleta kuchanganyikiwa kazini
  • Peana kazi / ripoti zenu kabla ya bosi wenu kuwauliza, uwe bora.
  • Fanya kazi ili ulipwe ,usilipwe ili kufanya kazi ,pesa isiwe motisha wako. Kazi inapaswa kuwa msukumo wako mkuu.
  • Epuka wafanyakazi wenzenu hasi, wapuuze na mfuate malengo yenu.
  • Kuweni wabunifu na tayari kufanya zaidi kila wakati. Utajisikia vizuri kuwa wa kipekee katika kampuni.
  • Kamwe usiamuru mshahara wako, kusanya unachopewa. Waonyeshe unachoweza kufanya  na baada ya miezi 3 ukae nao chini na uulize thamani yako .Makampuni hulipa thamani sio wakati wako. Jifunze maadili ya kampuni na uwe na majibu kwa vidokezo vyako.
  • SIWAHI KUBANDA / kunywa / kulala na wakuu wako. Usilale karibu na eneo lako la kazi, unahitaji mazingira mapya ya kufanya mambo yako! Fanya kazi pekee, hakuna mapenzi! endelea na Kazi! Fanyeni kazi pekee wapendwa wangu @veshashillan na @ rue.baby" Akothee aliwashauri mabinti wake.

Wiki iliyopita binti wa pili wa Akothee, Rue Baby alihitimu kutoka chuo kikuu cha Strathmore.