"Sina tabia, nitajirekebisha!" Zari Hassan akiri nusura amtongozee pasta wake kanisani

Muhtasari

β€’Mama huyo wa watoto watano ambaye kwa sasa anaishi Afrika Kusini  alifichua alivaa gauni lenye mpasuo mrefu akienda kuhudhuria ibada siku ya Jumapili.

β€’Kutokana na hayo mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz aliendelea kukiri kuwa amekosa tabia huku akiahidi  kujirekebisha.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara maarufu kutoka Uganda Zari Hassan nusura amtongoze mhubiri wake siku ya sabato.

Mama huyo wa watoto watano ambaye kwa sasa anaishi Afrika Kusini alitumia ukurasa wake wa Instagram kufichua alivaa gauni lenye mpasuo mrefu akienda kuhudhuria ibada siku ya Jumapili.

Zari alisema kilichomnusuru mchungaji wake dhidi ya  kuingia kwenye mtego ni kuwa alipofika kanisani hakufanikiwa kupata nafasi ya kukaa katika viti vya mbele.

"Nilijisahau nkawa nimevaa gauni lina mpasuo mrefuuu balaa. Uzuri nilipofika nikakuta viti vya mbele vimejaa. Bila ivo sjui ingekuaje? Maskini pasta!πŸ™ˆ" Zari alisema.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha yake akiwa yake akiwa amevalia gauni hilo lenye uwezo wa kualika majaribu kweli.

Kutokana na hayo mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz aliendelea kukiri kuwa amekosa tabia huku akiahidi  kujirekebisha.

"Sina tabia, ntajikerebisha" Alisema.

Wanamitandao walifurika chini ya chapisho lake Zari  Hassan kutoa hisia tofauti

@anita_wimbe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚zari una makusudi wewe muone

@fatma_lugogo Pastor angejuta πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

@marydimpoz1 Na nyeusi ulivaa ndani ama leo ilikua pinkπŸ˜‚

@riziki336 πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚wabongo mmefundisha mavyaa yangu vichambo😍😍😍😍😍😍love you mavyaa 😍😍😍