Watu wengi hawatakuunga mkono mpaka waone ni Maarufu kukuunga mkono -Diana Marua asema

Muhtasari
  • Bahati na mkewe wameingia  kwenye orodha ya wasanii wa Kenya ambao ni wanandoa na wamejitosa kwenye tasnia ya muziki
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Bahati na mkewe wameingia  kwenye orodha ya wasanii wa Kenya ambao ni wanandoa na wamejitosa kwenye tasnia ya muziki.

Diana bahati hivi majuzi alijiunga na tasnia ya muziki kama rapa na hadi sasa ametoa nyimbo mbili zinazovuma mitandaoni,na pia alitumbuiza baadhi ya maonyesho ya moja kwa moja.

Diana Bahati kupitia mtandao wake wa kijamii amemwambia mume wake kujenga himaya pamoja alisema haya baada ya kutoa nukuu muhimu.Anasema kuwa;

"Watu Wengi Hawatakuunga Mkono mpaka waone ni Maarufu kukuunga mkono 😉 Hebu Tujengehimaya mpenzi@BahatiKenya ❤️," Aliandika Diana.

Hisia zake ni za kweli kwa sababu hakuna mtu aliye tayari kukuunga mkono wakati wowote lakini atakuunga mkono kama njia ya kujitangaza.

Kwa bahati ni kinyume kwa sababu yeye amekuwa akimpa umaarufu mke wake hata kabla ya Diana kuanza kujitosa kwenye muziki na kujua yeye ni mwanamuziki anayependwa zaidi.