Diamond Platnumz apuuza siku ya kuzaliwa ya mwanawe na Zari Hassan, Prince Nillan

Zari aliweka wazi kwamba Nillan ndiye mtukutu zaidi kati ya watoto wake watano.

Muhtasari

•Kurasa zake za mitandao ya kijamii  zilisali tupu siku kutwa huku nyota huyo wa Bongo akionekana kutokuwa na neno la kuambia mwanawe.

•Mama Dangote alimkumbuka mjukuu wake kwa ujumbe maalum huku akimtakia maisha marefu.

Image: INSTAGRAM// PRINCE NILLAN

Mnamo siku ya Jumatatu (Desemba 6, 2021)  mtoto wa pili wa Diamond Platnumz na Zari Hassan, Prince Nillan aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Zari alisherehekea siku ile maalum kwa mwanawe na kumtakia Nillan kheri za kuzaliwa huku akiahidi kumpa malezi bora kulingana na njia za Mungu. Nillan ambaye ni kitinda mimba  wa Zari alihitimu miaka mitano.

Katika ujumbe wake wa kumtakia mwanawe kheri za kuzaliwa, Zari pia aliweka wazi kwamba Nillan ndiye mtukutu zaidi kati ya watoto wake watano.

"Heri ya siku ya kuzaliwa kwa Amigo mtukutu zaidi wa nyumba hiyo (nina shaka kuwa sikujua yeye ndiye😅) Siwezi kukupa ulimwengu, lakini nitakufundisha neno na njia za Mungu. Ukiweza kujifunza na kulijua hilo, dunia itakuwa yako. Mungu akubariki kwa ajili yangu @princenillan" Aliandika Zari katika ukurasa wake wa Instagram.

Matarajio ya wengi yalikuwa kwamba mzazi mwenza wa mwanasoshalaiti na mfanyibiashara huyo mzaliwa wa Uganda, Diamond Platnumz angepiga hatua kama ile na kuandikia mwanawe ujumbe maalum katika kurasa zake za mitandao ya jamii.

Hata hivyo kurasa zake za mitandao ya kijamii  zilisali tupu siku kutwa huku nyota huyo wa Bongo akionekana kutokuwa na neno la kuambia mwanawe.

Hata hivyo mama yake Diamond,  Mama Dangote alimkumbuka mjukuu wake kwa ujumbe maalum huku akimtakia maisha marefu.

"Wale twaruka @princenillan Maisha marefu yenye baraka tele 🎂🎂🎂" Aliandika Mama Dangote katika ukurasa wake wa Instagram.