'Heshima yako kwa wanawake iko wapi?,'Diana Marua amuuliza Willy Paul baada ya kufichua alijaribu kumbaka

Muhtasari
  • Diana Marua ametumia chaneli yake ya youtube kufichua kwamba Mwimbaji Willy Paul almaarufu Pozze alijaribu kulala naye kwa lazima miaka michache iliyopita
Diana Marua
Image: Hisani

Diana Marua ametumia chaneli yake ya youtube kufichua kwamba Mwimbaji Willy Paul almaarufu Pozze alijaribu kulala naye kwa lazima miaka michache iliyopita.

Kulingana na Diana ilimchukua muda mrefu kudhihirisha kwa umma kwa sababu wakati huo hakuwa na sauti na hakuna mtu ambaye angemwamini.

Willy Paul pia ni mtu mashuhuri wa Kenya na msanii, amekuwa akimkejeliDiana Marua baada ya kutoa nyimbo zake mbili , alidai kuwa Diana Marua hajui jinsi ya kkuimba vizuri.

Mastaa hao wawili leo wanavuma mitandaoni, baada ya mwimbaji Diana Marua kufichua Willy Paul alijaribu kumbaka miaka michache iliyopita.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Diana alizidi kumuuliza Paul Heshima yake kwa wanawake alipeleka wapi, na kusisitiza kwamba watafika mahakamani.

"Nimekuwa Nikilia Tangu Nilipofunguka katika Video hii; hii Ilikuwa Siku Mbaya Zaidi Katika Maisha Yangu na Wakati wa Kutisha kwa Mwanamke Yeyote Aliyekumbana na Kubakwa au karibu kubakwa

Bado siamini kwamba Mwanaume Anaweza Kujaribu Kukubaka kwa nguvu lakini kwa sababu wamegundua ulienda Kimya bado anatafuta kiki na Jina Lako Wakidanganya hadharani kuwa wamelala na Wewe kwa ajili ya Kujishughulisha tu

Je huo ni Uthibitisho wa Ulichokifanya??? 😭😭😭 Unavuka hata Mipaka na kuimba juu yake ili kutafuta kiki kwa ajili ya kuokoa Nambari na Kazi yako ambayo tayari imekufa???

Unakosaje Heshima kwa Kiwango hicho??? Unathubutu hata Kuwataja Watoto Wangu katika Upuuzi wako??? Heshima yako kwa akina mama na wanawake iko wapi???," Aliandika Diana.

Alizidi na ujumbe wake na kusema kuwa;

"Je, ndivyo unavyomkosea heshima Mama yako??? 😭😭😭 Nilikuwa Kimya Kuangalia na Kukusanya Ushahidi unaohitajika kwa Kesi 3 nilizofungua Polisi Mahakamani... Wanawake Wote Hawa uliowabaka na Kujaribu Kuwabaka tayari wapo kwenye DM zangu na Kwa ushawishi alionipa Mungu

Nitahakikisha wote wanapata Haki; wanawake wengi wamekuwa Kimya kwa sababu anawatishia Kujua Watu Wakubwa Serikalini Wacha Sasa Tuone-sasa ni wakati wa kusimama kwa ajili ya wanawake wetu."