Mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu kama Amber Ray amejitongeza kuzungumzia uvumi kuhusu kilichosababisha kifo cha rafiki yake wa dhati.
Amber Ray ametumia ukurasa wake wa Instagram kupuuzilia mbali madai kwamba rafikiye @empresal aliaga kutokana na matatizo ya mwili yaliyosabibishwa na sindano ya kubadilisha rangi ya ngozi.
Mama huyo wa mtoto mmoja ameweka wazi kwamba marehemu alizaliwa akiwa mrembo kama alivyokuwa wakati kifo kilimjia na hajawahi kufanya mabadiliko ya rangi ya ngozi yake, kinyume na madai ya baadhi ya wanamitandao.
"Sijawahi kuwa mtu wa aina ya kuzungumzia uvumi lakini nataka tu kuweka wazi kuwa BFF wangu hakufa kutokana na sindano ya kuchumbua ngozi kama vile nyinyi wavivu mnavyodai. Alizaliwa akiwa mweupe na mrembo sana" Amber Ray alisema.
Alisema uchunguzi wa maiti tayari umefanyika kubaini kilichoangamiza rafikiye na kinachosubiriwa kwa sasa ni matokeo.
Amber Ray amewasuta vikali wanaoneza uvumi kuhusu kilichosababisha kifo cha rafikiye huku akisisitiza hakuna yeyote anayejua ukweli.
"Hata sisi watu wa karibu hatujui kilichomuua na sembuse wewe ambaye hamkuwa mnajuana. Unaongea hapo kama k*t*mb* mwene etoo. Aibu kwenu!" Aliandika.
Amewashuku wote ambao wamekuwa wakimjulia hali na kumtumia jumbe za kumfariji tangu alipopoteza rafikiye huku akieleza anajiskia vizuri sasa.