Hapana sijazaa na Diamond,'Msanii Malkia kutoka Tanzania aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Hii ni baada ya kusema kuwa hana mtoto na Diamond Platnumz jinsi watu wanavyosema
  • Usemi wake Karen umeibua hisia tofauti mitandaoni, huku akifichua kwamba ataolewa akiwa na miaka 40
Msanii Malkia Karen
Image: Malkia/INSTAGRAM

Malkia Karen ambaye ni mwimbaji maarufu wa Tanzania ameibua hisia kwenye mitandao tofauti ya kijamii.

Hii ni baada ya kusema kuwa hana mtoto na Diamond Platnumz jinsi watu wanavyosema.

Kulingana na majibu ambayo mwimbaji huyo alimtolea shabiki, Karen alikuwa akisema kuwa hana mtoto na Diamond na watu waache kuwahukumu vibaya.

Usemi wake Karen umeibua hisia tofauti mitandaoni, huku akifichua kwamba ataolewa akiwa na miaka 40.

"Ni kweli umezaa na Diamond," Shabiki aimuuliza Malkia.

"Hapana," Alijibu.

Pia shabiki mwingine alimuuliza kwa nini aliamua kuzaa kabla ya kuolewa ambapo Malkia alijibu na kuwmambia.

"Nimepanga kuolewa tena sana kuanzia miaka 40 kuendelea, na kiasayansi haufai kuzaa miaka hiyo kama huna matatizo yeyote," Malkia alijibu.