Hakutaka kuheshimu kazi yangu,'Hatimaye Masauti azungumzia madai ya kufurushwa jukwaani Mombasa

Muhtasari
  • Akizungumzia suala hilo, Masauti aliwanyooshea vidole waandaaji na kukataa kumlaumu Mbosso kwa kilichoshuka.
Masauti
Masauti

Masauti amejitokeza kuzungumzia madai kuhusu jinsi yeye na msanii mwenzake, Nadia Mukami walivyodhulumiwa jukwaani wakati wa onyesho la 'Mbosso bright future' wikendi iliyopita mjini Mombasa.

Hata hivyo, ripoti zilizotoka kwenye onyesho hilo zilidai kuwa Masauti na Nadai walidhulumiwa na waandaji wa onyesho hilo ambao hawakutaka wamalize maonyesho yao na kuwaacha wawili hao wakiwa wamekata tamaa na mashabiki wao kuchanganyikiwa.

Akizungumzia suala hilo, Masauti aliwanyooshea vidole waandaaji na kukataa kumlaumu Mbosso kwa kilichoshuka.

Anasema mwanamke mmoja 'hakutaka kuheshimu sanaa yangu na kuonyesha thamani yangu kama msanii wa nyumbani.'

"Sijataka kuongelea issue ya show ya Mombasa lakini pia nimeona nivunje ukimya ili kuepuka unafki

Najua mashabiki zangu wanahofu kutaka kujua what exactly happened ndio singependelea mtu atumie jina langu kuelezea my side of the story

Nataka niwaombe tu kwanza tukio hili lilitokea lisitumike kumharibia rafiki yangu @mbosso_ jina wakati siye aliyeandaa show hii

Makosa yatupiwe waandalizi wa show hio mchwara tena sio wote ni dada mmoja tu ambaye singependa nimtaje jina😏Yeye ndo hakutaka kuheshimu kazi yangu na kunionyesha thamani kama msanii wa nyumban

Lakini kama mpambanaji niliamua kueka kazi kwanza maana sipendi kueka hisia zangu mbele kwakua nina familia nyuma inayoniangalia mimi tu

Siku ile ya show walienda kinyume na mahitaji yangu kwenye rider lakini wala sikuvunjika moyo kwakua ni kijana ninayepambania sanaa yangu ili familia yangu ipate rizki😣

Hakukua ata na usafiri wangu ili kufika sound check. Kuelekea mda wa show pia vilevile niliona hakuna mabadiliko yoyote. Kwasababu zao tu waliamua kuenda kinyume na rider iliyoeka wazi mahitaji yangu yote hadi kukatiza mawasiliano

Sikueka kichwa chini hata kidogo ndio management yangu ikafanya mpango wa usafiri ili tufike kwenye show kwani mashabiki zangu ni watu muhimu sana kwangu," Alisema Masauti.

Pia alifichua vile mtangazaji Mzazi Willy Tuva aliingilia kati na kufanya shoo yao iendelee.

"Nilifika kwenye location nikasubiri hadi mda wangu wa kupanda stage kuperform. Baada ya kama nusu saa hivi, nikiendelea kuperfoem nikaona nyuma kuna mvutano unaendelea kati ya management yangu na watu kwenye stage. Yuleyule dada alitaka kunikatiza show katikati😒Vita hivo viliendelea kati yao na uongozi wangu ambao ulipinga hilo wazo lao la kusmamisha show katikati. Dj alismamisha show kwasababu yule dada alimtishia kutomlipa🤬 mvutano uliendelea akaja @mzaziwillytuva aliyeingilia kati na kukataa mziki ukatishwe namna hio. Aliungana nasi show ikaendelea. Nikaimba na mashabiki zangu hadi wakati wangu ukaisha ndo nikashuka kwenye stage."