Orodha ya watu mashuhuri walioachana mwaka wa 2021

Muhtasari
  • Orodha ya watu mashuhuri walioachana mwaka wa 2021
  • Sio watu tu wa kawaida bali watu mashuhuri waligonga vichwa vya habari mitandaoni baada ya baadhi yao kuachana
Image: INSTAGRAM//GOVERNOR ALFRED MUTUA

Mwaka wa 2021 umekuwa na mambo mengi ikiwemo watu kufunga pingu za maisha huku baadhi yao wakitemana hadharani.

Sio watu tu wa kawaida bali watu mashuhuri waligonga vichwa vya habari mitandaoni baada ya baadhi yao kuachana.

Ni mahusiano ambayo wengi na wanamitandao waliamini kwamba hayatakamilika, kwani walionyesha mapenzi yao kila kuchao.

Katika makala haya tutazingatia na kuangazia watu mashuhuri ambao waliachana na kutemana mwaka wa 2021;

1.Gavana Alfred Mutua na LIlian Ng'ang'a

Gavana wa Machakos na Mutua na aliyekuwa mkewe Lilian Ng'ang'a walijitokeza hadharani na kutangaza kutengana kwao baada ya kuwa pamoja kwa miaka 10.

Image: INSTAGRAM//GOVERNOR ALFRED MUTUA

2.BenPol na Anerlisa

Wawili hao walikuwa wakupigiwa mfano, kwani walionyesha mapenzi yao mitandaoni,kutengana kwao kulifahamika baada ya Benpol kumpa Anerlisa talaka Machi 2021, miezi 12 baada ya harusi yao.

gVUk9kpTURBXy80NTA3YjEwNDQxOGFhMDQ1MTFlOGFiZDU2NDk5MDJiZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
gVUk9kpTURBXy80NTA3YjEwNDQxOGFhMDQ1MTFlOGFiZDU2NDk5MDJiZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

3.Mulamwah na Caro Sonie

Mchekeshaji Mulamwah waliachana na mpenzi wake Sonie miezi miwili baada ya kubarikiwa na kifungua mimba wao.

Mulamwah na Caro Sonie
Image: INSTAGRAM/CARO

Huu ulikuwa mwaka wao kusema kwamba yametosha na uachana, huku wakikubaliana kumlea mtoto wao.

4.Nviiri story teller na Elodie Zone

Elodie alitangaza kutengana kwa moyo na Nviiri. Kabla ya kutangaza kuvunja ndoa hiyo, alimshutumu Nviiri kwa kumdhulumu kimwili, kiakili, kwa maneno na kihisia walipokuwa wakichumbiana.

Tunatumai kwamba watawapata wapenzi wa maisha yao.