Mchekeshaji Erick Omondi jumanne amejitokeza na kutetea kauli yake kwamba muziki wa bongo flavour ambao umefanya waimbaji wengi wa Tanzania wavume ameanza kupotea.
Kupitia mtandao wake wa Instagram, Omondi amemjibu zuchu ambaye alikuwa anapuzilia mbali maneno ya muigizaji huyo, huku akisema wanamuziki wa Tanzania wameamua kuwa na mtindo mpya ambao utawasaidia kujulikana nje ya eneo lao.
"Bongo flavour haiwezi kufa. wasanii wanatoka nje ya eneo lao, kutafuta utofauti wa kujaribu sauti mpya. haijawahi shuhudiwa kuua tasnia yoyote, tasnia ya muziki ni kubwa sana, wacha msanii ajaribu mambo yao. Hayo ni mabadiliko" Zuchu alisema
Kufuatia kauli hio Eric Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake huku akimjibu staa za huyo wa Bongo na kumweleza kwamba wanamuziki wa Kenya walianza hivyo na mziki wao ukapotea
"Dada yangu mpendwa, hivi ndivyo inavyoanza, huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake.Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea" Omondi alisema
Aliendelea kueleza madhara ambayo yanaweza sababishwa na mtindo wa Amapiano na kusema mtindo huo ni kama Basi ambalo linapita na kuwaonya wasipojichunga linaweza kuwabeba na mtindo wao kusahaulika.
"Bongo flavour iko SAWAA kabisa na hakuna haja ya kuwaacha Bongo Fleva ati kwa ajili ya 'diversify' Amapiano ni Basi tu linapita ila sisi tundapanda bila kujua linaenda wapi, tutashindwa kurudi nyumbani.tutakuwa tunauza sera zao na kushindwa kurundi nyumbani. tutakuwa tunauza tamaduni zao na kuua zetu za nyumbani" Mchekeshaji Omondi alinakiri
Isitoshe alipongeza Zuchu kwa wimbo alioimba wa 'Sukari' ambao uliwavutia sana kwa mdundo wa wake na pia sauti nyororo iliyoimba.
"Unapoimba 'Sukari' kwa sauti hiyo tamu ya kweli ya bongo na mdundo . unachofanya kimsingi ni kuinua na taifa na Bendera ya Tanzania"