Dr Dre kumlipa mkewe shilingi bilioni 11 baada ya kumpa talaka

Muhtasari

•Dr Dre baada ya kutafuta suluhisho ya talaka na mke wake Nicole Young, wamekubaliana rasmi kuvunja  ndoa ambayo iliyodumu kwa takribani miaka 25.

Dr. Dre na mkewe Nicole Young
Dr. Dre na mkewe Nicole Young
Image: Hisani

Mtayarishaji muziki maarufu duniani, Andre Romelle Young almaarufu Dr Dre baada ya  kutofautiana na  mke wake Nicole Young, wamekubaliana rasmi kuvunja  ndoa ambayo iliyodumu kwa takribani miaka 25.

Dr Dre ambaye ana umri wa miaka 56 amefikia na mkewe kuvunja mahusiano yao, hatua ambayo itamgharimu kiasi cha dola million 100 za Kimarekani ambazo ni sawa na Bilioni 11 za kenya

Hapo awali wanandoa hao wa zamani ambao wamekuwa wakipigana vikali kuhusu pesa za  nguli huyo wa Muziki walikubali kuivunja ndoa kisheria kutokana na tofauti zilizojitokeza baina yao.

Kwa kupitia mtandao wa TMZ,Nicole atapokea dola bilioni 50 kwa sasa,na nyongeza ya dola milioni 50 ndani ya mwaka mmoja, ambayo ni jumla ya dola milioni 100

Dre walioana na Nicole mwaka wa 1996 na kubarikiwa na watoto wawili, Truice Young  na Truly Young. Truice Young ambaye ana miaka 24 na dadake yake Truly Young, 20.

Ilisemekana wakati wawili hao waliachana Dre alifanya sherehe ya kusherekea talaka yao.

Suluhu hio itahitimisha vita vilivyoanza  mwaka wa 2020 baada ya Nicole kuwasilisha talaka kwa mwanamuziki huyo akitaja tofauti zao hazingeweza kusuluhishwa.Alieleza kuwa mwanamuziki huyo alifukuza nyumba yao na kumfanyia vitendo hivyo vya kidhuluma

Rapa huyo mashuhuri ataweza kuhifadhi mali zake nyingi zikiwemo Ksh 10 bilioni ($100 milioni) estate ya Brentwood, nyumba ya Malibu, nyumba 2 huko Calabasas, na mali sehemu 4 katika eneo la L.A