Eric Omondi asema Muziki wa kenya umekufa

Muhtasari

ā€¢aliongeza kusema Mwanamuziki ambaye anayemheshimu na kuvulia kofia kwenye  kanda ya Afrika Mashariki ni Diamond ambaye kwa Miaka mingi amekuwa ameshikilia muziki wa kanda hio na kuuweka kwenye ramani ya kimataifa.

Mchekeshaji Eric Omondi
Mchekeshaji Eric Omondi
Image: Hisani

Mchekeshaji Eric Omondi siku ya Jumanne alijitokeza na madai kwamba muziki wakenya umekufa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Omondi alisema ni jambo la kushangaza sana kuona Kenya ikisifia mtoto wa miaka 14, ambaye amejitosa kwenye tasnia ya muziki, Trio Mio.

"Chenye Kenya inaweza kuwasilisha  kwa muziki wa Afrika ni Trio Mio, mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 14 ambaye hajawahi kutoka  kenya" Omondi alinakili kwa ukurasa wake

Isitoshe aliongeza kusema Mwanamuziki ambaye anayemheshimu na kuvulia kofia kwenye  kanda ya Afrika Mashariki ni Diamond ambaye kwa Miaka mingi amekuwa ameshikilia muziki wa kanda hio na kuuweka kwenye ramani ya kimataifa.

"mwanamuziki pekee wa afrika mashariki ninayemkubali ni Diamond Platinum let give credit where its deserve chibu anajaribu kweli.tumpe sifa pale inapostahili, Sauti Sol wanajaribu lakini bado" Omondi alisema

Aliwapa changamoto  waimbaji wa Afrika mashariki huku akitumia mifano ya Wizkid ambaye alijaza 02 Arena kwa siku 3 mfululizo , huku Burna boy akitunzwa kila mwaka kwa kuibuka mwanamuziki bora kwenye tunzo za Grammy award.