'Nilifunga nguo zangu mara nyingi tayari kuondoka!,' Mpenzi wa Baha afunguka kuhusu mahusiano yao machanga

Muhtasari

•Malkia huyo mwenye umri wa miaka 21 amefichua kwamba walipoanza kuishi pamoja alipanga nguo zake mara nyingi akikusudia kuondoka baada yao kuzozana. 

•Georgina alisema mahusiano yao si ya kubebeshana mizigo, alisema yanahusisha kusaidiana katika mambo mbalimbali ya kinyumbani kadri mtu awezavyo.

Image: INSTAGRAM// GEORGINA NJENGA

Bi Georgina Njenga ambaye ni mpenzi wa mwigizaji Tyler Mbaya almaarufu kama Baha  amefichua kuwa mahusiano yao yamekuwa yakikabiliwa na changamoto mara kwa mara.

Alipokuwa anashirikisha wafuasi wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, Georgina alisema kama hali ilivyo katika mahusiano mengine wa kawaida, kumekuwa na mabishano katika mahusiano yao pia kwa wakati mmoja au mwingine.

Malkia huyo mwenye umri wa miaka 21 amefichua kwamba walipoanza kuishi pamoja alipanga nguo zake mara nyingi akikusudia kuondoka baada yao kuzozana. Hata hivyo mpenzi wake angemzuia kuondoka kila mara na wangetafuta suluhu ya mzozo wao pamoja.

"Mabishano huwepo na aghalabu huwa kuhusu mambo madogo zaidi kuwahi kutokea. Lakini daima tunatafuta suluhu. Mara ambapo nilifunga nguo tulipoanza kuishi pamoja heeh, lakini alikuwa anahakikisha sijaenda" Georgina alijibu shabiki aliyetaka kujua mambo ambayo amejifunza katika kipindi ambacho wameishi pamoja na Tyler.

Georgina alisema mahusiano yao si ya kubebeshana mizigo, alisema yanahusisha kusaidiana katika mambo mbalimbali ya kinyumbani kadri mtu awezavyo.

Pia alifichua kwamba wakati ufikapo wanatazamia kupata angalau watoto watatu ama wanne iwapo uchumi utawaruhusu.

"Kama ulivyosema ni mwenzangu. Anasaidia kadri anavyoweza katika kazi za nyumbani lakini mimi hufanya zaidi. Ninasaidia pale ninapoweza kifedha lakini yeye hufanya zaidi" Georgina alijibu shabiki aliyetaka kujua jinsi wanavyoshirikiana katika mahusiano yao.

Wawili hao wawili walianza kuchumbiana mapema mwaka uliopita na wamekuwa wakiishi pamoja tangu wakati huo.