"Sitaki mubaba akufie mikononi mwangu!" Carol Sonnie azungumzia mahusiano baada ya kutengana na Mulamwah

Muhtasari

•Mama huyo wa mtoto mmoja aliweka wazi kwamba  yuko sawa kuchumbiana na mwanamume mwenye umri wa ujana kwa kuwa wana mengi ya kufanana.

•Muthoni aliongeza kuwa anakusudia kutengeneza utajiri  pamoja na mume wake mwenyewe wala sio kujinufaisha na mali ya mume wa mwingine.

Mulamwah na Caro Sonie
Image: INSTAGRAM/CARO

Bi Caroline Muthoni almaarufu kama Carrol Sonnie na ambaye alikuwa mpenzi wa mchekeshaji Mulamwah ameapa kwamba hawezi kuchumbia mwanamume mzee (mubaba) kwa sababu ya fedha.

Alipokuwa anajibu maswali ya mashabiki wake kupitia YouTube channel yake, mwigizaji huyo aliweka wazi kwamba  yuko sawa kuchumbiana na mwanamume mwenye umri wa ujana kwa kuwa wana mengi ya kufanana.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema hawezi kubali kujitosa kwenye mahusiano na 'mubaba' kwani anahofia asije akakufia mikononi mwake.

"Naweza kuchumbiana na kijana. Hii ni kwa sababu tunaendana na sitaki mvutano. Sitaki mubabez akufie kwa mikono yangu . Sitaki kuridhi mali ya wenyewe nikiwa mdogo hivi!" Muthoni alisema.

Muthoni aliongeza kuwa anakusudia kutengeneza utajiri  pamoja na mume wake mwenyewe wala sio kujinufaisha na mali ya mume wa mwingine.

"Nataka kujenga himaya na mume wangu mwenyewe, sio na mume wa mwingine. Ndio maana siwezi kuchumbia mubaba" Muthoni alisema.

Mwigizaji huyo alikiri kwamba mtu mashuhuri anayempenda sana ni mwanamuziki  wa Pop Jason Derulo.

Pia alifichua kuwa angepata nafasi ya kuhama nchi ya Kenya angependa kuishi katika nchi jirani ya Tanzania.