Carrol Sonnie afunguka kuhusu hali yake ya mahusiano ya sasa baada ya kutengana na Mulamwah

Muhtasari

•Alisema kwa sasa hayuko tayari kujitosa kwenye mahusiano mengine licha ya kuwa amekuwa akipokea jumbe nyingi za maombi kutoka kwa 'wababa'.

•Muthoni  pia  aliweka wazi kwamba Mulamwah ndiye baba mzazi wa binti yake na kupuuzilia mbali madai ya baadhi ya wanamitandao kwamba mtu mwingine alihusika.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa mchekeshaji Mulamwah, Caroline Muthoni almaarufu kama Carrol Sonnie amefunguka kuhusu hali yake ya mahusiano ya sasa hivi takriban mwezi mmoja baada ya kuthibitisha kutengana  kwao.

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu kwenye chaneli yake ya youtube alikomshirikisha Mungai Eve, Muthoni aliweka wazi kwamba kwa sasa hachumbiani na yeyote yule.

Mama huyo wa binti mmoja alisema kwa sasa hayuko tayari kujitosa kwenye mahusiano mengine licha ya kuwa amekuwa akipokea jumbe nyingi za maombi kutoka kwa 'wababa'.

"Sichumbiani na mtu yeyote. Sidhani nitachumbiana na yeyote hivi karibuni. Siko tayari.. Kuna wababaz wamekuwa wakislide kwa DM, ni wengi. Lakini mimi sitaki. Kwa sasa sitaki kuangazia mtu mwingine ila mtoto wangu pekee" Muthoni alisema.

Mwigizaji huyo alikiri kwamba katika kipindi ambacho alikuwa kwenye mahusiano aligundua kuwa mahusiano sio rahisi.

"Mapenzi usicheze nayo. Mapenzi ni ya wazungu. Wachia wazungu" Alisema.

Muthoni  pia  aliweka wazi kwamba Mulamwah ndiye baba mzazi wa binti yake na kupuuzilia mbali madai ya baadhi ya wanamitandao kwamba mtu mwingine alihusika.