"Atafute bibi, nyumba yake chafu inahitaji mwanamke!" Mr Seed ampasha Ringtone baada yake kumkosoa

Muhtasari

•Mr Seed alisema muda umewadia Ringtone kutafuta mke huku akimshtumu kwa kushindwa kutunza nyumba yake.

•Aliwahakikishia mashabiki wake kwamba hajagura injili kama alivyodai Ringtone.

Mr Seed, Ringtone Apoko
Mr Seed, Ringtone Apoko
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Moses Tarus Omondi almaarufu kama Mr Seed amemkosoa sana mwenzake Ringtone Apoko kwa kumbandika jina  'mkubwa wa washerati' baada yake kutoa wimbo wa mapenzi.

Alipokuwa anahutubia wanahabari hivi majuzi, Mr Seed alisema Ringtone hafai kunyooshea wengine vidole na kudai kwamba amekuwa akinyemelea wanadada wengi hapa nchini.

Mr Seed alisema muda umewadia Ringtone kutafuta mke huku akimshtumu kwa kushindwa kutunza nyumba yake.

"Yeye ndiye mkubwa wa Washerati. Ringtone hakosi kwa DM ya msichana yeyote hii Nairobi. Aache kushinda amenyoosheana vidole, kwanza atafute bibi aoe. Juzi niliona mmekuwa kwa nyumba yake, nyumba chafu inahitaji mwanamke. Jokovu limeoza, microwave imeoza, anapika sukuma. Mwambieni atafute bibi 2022 atulie. Bibi atamueka laini, hii mdomo ako nayo hatakuwa nayo. Atakuwa anaongea hivi anakumbuka akirudi kwa nyumba atapigwa. Huyo anaweza kaliwa na mwanamke!" Alisema Seed.

Mr Seed aliwahakikishia mashabiki wake kwamba hajagura injili kama alivyodai Ringtone. Alisema angali anasambaza maneno mazuri kupitia kwa muziki wake.

"Wokovu ni binafsi kwa kila mtu. Mimi ni msanii, mimi ni msanii wa injili, bado nasambaza wema. Ama Ringtone akienda kutafuta mwanamke atasema Mungu ameniambia wewe ndio bibi yangu? Hawezi! Nina hakika hao wasichana wake huwa anawachezea 'Dawa ya baridi' hapo" Seed alisema.

Alisema kwamba amejitolea kumsaidia Apoko kwa kufanya collabo naye ili angalau apate kazi ya kufanya aache udaku.