Burna Boy na Shatta wale wapanga vita kumaliza uhasama baina yao

Burna Boy
Image: Hisani

Mwanamuziki  Charles Armah almaarufu kama Shatta Wale kutoka Ghana amekubali ombi la Burna Boy  la kupigana masumbwi ili kumaliza ugomvi wao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitte, Wale alinakiri ujumbe uliokuwa unaelekezwa kwa  msanii huyo mwenzake  kutoka nchi ya Nigeria huku akimtaarifu kwamba yuko tayari kwa pambano hilo na kupendekeza uwanja wa Accra, Ghana eneo badala la pambano hilo.

"Oh @burnboy unasema unataka kuzichapa na mmi  moja kwa moja  ..sawa tulifanye kwenye  uwanja huu wa michezo wa Accra! " alisema Shatta Wale.

Ata baada ya kukubaliana kupigana na Burna Boy ,mwanamuziki huyo aliendelea kumshambulia na kufichua mambo ya  siri ambayo alidai Burna Boy alifanya wakati ule walikuwa na uhusiano mwema baina yako.

Isitoshe alieleza haja yake kuu ya kutumia mitandao ya kijamii ni kujibizana na wanamitandao aliotaja kutoelewa kinachoendelea.

"Twitter ni mahali ninapenda kuongea na wapumbavu sana kwa sababu  wengi wa watu  hapa wanafikiri wana akili, lakini maskini katika maisha halisi Nenda utafute kazi ya mashabiki wavivu wa Nigeria wa 'toy' ya Burna" Shatta alisema