'Mume wangu hajanigusa kwa miaka 4,'Kipusa aeleza masaibu anayopitia kwenye ndoa

Muhtasari
  • Kipusa aeleza masaibu anayopitia kwenye ndoa
  • Kulingana na Suzanna mumewe alimpenda mwaka mmoja kwenye ndoa, na kutekeleza mambo ya ndoa pamoja hadi tenddo la ndoa
Side view of young woman with eyes closed
Side view of young woman with eyes closed

Ni matamanio ya kila mwanamke na mwanamume kumta mwenzi ambaye ana hisia zake na anmpenda katika kila jambo.

Wengi wanashindwa mbona idadi ya 'single mothers' na kuitwa 'baby daddy' inazidi kuongezeka kila kuchao, ukweli ni kwamba wengi waliona kwamba hawawezani na ndoa baada ya kufunga pingu za maisha.

PIa kuna wale wamekuwa wakiwatafuta mipango wa kando, ikiwalazimu wenzao  kukata tamaa na kupeana talaka.

Ninapozungumzia kuhusu masaibu na cangamoto za ndoa ambazo wengi wamekua wakivumilia badala ya kutoroka ndoa yao, siwezi msahau Suzanna kipusa ambaye amekuwa kwa ndoa kwa miaka 5.

Kulingana na Suzanna mumewe alimpenda mwaka mmoja kwenye ndoa, na kutekeleza mambo ya ndoa pamoja hadi tenddo la ndoa.

Lakini miaka 4 nini kilichotokea?Huu hapa usimulizi wake'

"Jambo ambalo naweza kuwaambia wananddoa wachanga ndoa sio jambo la kukimbilia wala kutania kwa maana ndoa inachangamoto zake

Ninapozugumzia changamoto, mume wangu hajawahi nigusa kwa miaka 4 licha ya kudai ananipenda, tunalala kitanda kimoja, nikimuuliza kama hisia zake kwangu ziliisha hanijiu chochote

Tumebarikiwa na mtoto mmoja, ndio amekuwa akitekeleza majukumu yote lakini kinachoniuma ni kuwa tukienda kitandani hafanyi chochite ata kunigusa, nimevumia kwa miaka 4 sasa ni mwaka mwingine, nitoke kwenye ndoa hii ama nifanye aje

Kwa maana hamna mtu ambaye anaweza ishi bila tendo la ndoa ilhali yuko kwenye ndoa, huo sio uungwana kwangu, sijui kama yuko na mipango ya kando ambayo inamfanya asiniguse," Alieleza Suzanna.