'2022 Wanaume tupunguze mshene,'Arrow Bwoy asema baada ya habari za Nadia kuwa mjamzito kufichuliwa

Muhtasari
  • Arrow Bwoy asema haya baada ya habari za Nadia kuwa mjamzito kuenea
  • Habari hizo zimepokelewa na hisia tofauti miandaoni huku baadhi ya mashabiki wakiwapongeza wawili hao
Arrow Bwoy
Image: Maktaba

Msanii Arrow Bwoy ameoneana kugadhabishwa na habari zilizofichuliwa na mcheshi Jalang'o kuwa mpenzi wake Nadia ana ujauzito wake.

Katika kipindi chake cha asubuhi  kwenye Kiss FM, Jalang’o alimtaka Mukami kukoma kuficha madai ya ujauzito wake kwa kuvaa masweta ya kubebea akiongeza kuwa ujauzito huo ungeonekana hivi karibuni.

“Nadia pia sasa itabidi awache kuvaa masweater…wacha mimba tu itoke tu…mimba ni kama kohozi hauwezi zuia, ikibidi ukohoe utakohoa tu..”

Arrow Bwoy alijibu habari hiyo kwa maneno makali.

"2022 wanaume tupunguze mshene bana biashara haikuhusu achana nayo kabisa shugulika na maisha yako," Msanii huyo alisema.

Habari hizo zimepokelewa na hisia tofauti miandaoni huku baadhi ya mashabiki wakiwapongeza wawili hao.

Siku chache zilizopita, mmoja wa mashabiki wa Nadia alimuuliza ujauzito wake uko wwapi baada ya kupakia picha mitandaoni ambapo Nadia alimjibu na kusema kuwa;

"hebu tuulize Ronaldo ni kama tumeiacha kwa field kesho siataisahau nitakuletea unibebee nisiisahau tena.”