Chris Kirwa amshauri Holy Dave kuoa kabla siku ya Valentine

Muhtasari
  • Chris Kirwa amshauri Holy Dave kuoa kabla siku ya Valentine
Holy Dave
Holy Dave
Image: Hisani

Mratibu wa hafla Chris Kirwa  Jumanne alimshauri mwimbaji wa Injili Holy Dave  kuhakikisha ameoa kabla siku ya  wapendao 'Valentine'

Kupitia ukurusa wa Instagram wa Holy Dave, kwenye sehemu ya maoni, Chris kirwa  alinakili kwamba atafute mke ili ifikiapo siku ya wapendanao awe  angalau na mtu wakushauriana naye.

" Indomie iwezi kusaidia,Tafuta mtu nani, baridi ya Valentine inakaribia." Kirwa aliandika kwenye sehemu ya maoni ya Holy Dave

Kufuatia kauli hiyo, Holy Dave alijitokeza na kujibu kwa ucheshi kwamba Chris kirwa ameamua kumtoanisha mwaka  huu mpya, huku akiwa pongeza Gardian Angel kwa kufunga ndoa na  mpenzi wake wa siku nyingi  Esther Musila.

Aidha, aliwambia mashabiki wake pia yeye ako njiani kupata mchumba.

"Hizi  vita  mnaanza nazo 2022 staki. HD hapangwingi. lakini mbona uongo. Valentine hainipati hivi... Hongera kwa Esther Musila na Gardian Angel, Mimi ndiye nafuata sasa" Holy Dave alisema kupitia ukurusa wa instragram

Holy Dave anafahamika sana mitandaoni kutokana na upishi wake, ambao amekuwa akipakia kwenye ukurasa wake wa instagram kwa muda sasa.

Pia ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao maisha yao ya mapenzi hayajakuwa mitandaoni.