Muigizaji wa Hollywood na Mshindi watuzo ya Oscar,Lupita Nyongo amepimwa na kukutwa na virusi vya uviko-19
Lupita, kupitia ukurasa wake wa twitter, Jumanne alipimwa na kupatikana na virusi hivyo vya Korona licha ya kupata chanjo.
Katika tangazo hilo alisema kwa sasa amejitenga na watu kuzuia kueneza virusi hivyo na akasema anatarajia kupata nafuu hivi karibuni.
" Mimi pia nimethibitishwa kuwa na Covid-19. nimechanjwa kikamilifu. nimejitenga na ninaamini nitakuwa mzima."
Lupita aliwaomba mashabiki wake watahadhari na virusi hivi vya Korona "Tafadhali fanya yote uwezayo ili kujilinda wewe na wengine dhidi ya magonjwa hatari."
Kutokana na virusi hivyo, Hollywood imelazimika kuhairisha majojiano ya matangazo ya filamu mpya 'The 355' ilikuzingatia kupona kwa nyota wao
I too have tested positive for COVID-19. I'm fully vaccinated and taking care in isolation, so I trust I will be well. Please do all you can to keep yourself and others protected from serious illness. #StayMaskedAndVaxxed
— Lupita Nyong'o (@Lupita_Nyongo) January 4, 2022
Lupita ni miongoni mwa waigizaji waliotarajiwa katika Tamasha la kusisimuliwa lililotarajiwa kufanyika Ijumaa. Wengine waliokuwa kuwa kwenye orodha hio ni ikiwemo na Jessica Chastain, Penelope Cruz, Diane Kruger, na Bingbing Fan.