(+Picha) Jinsi ilivyokuwa katika harusi ya Guardian Angel na Esther Musila

Muhtasari

•Guardian Angel kwa wakati huo alionekana kuwezwa na hisia na kutiririkwa na machozi ya furaha

Guardian Angel amvisha pete Esther Musila
Guardian Angel amvisha pete Esther Musila
Image: DRACO SHOT

Hatimaye Guardian Angel na Esther Musila walifunga pingu za maisha siku ya Jumanne katika hafla ya faragha iliyofanyika katika uwanja wa Sue Gardens eneo la Muthaiga.

Wapenzi hao wawili ambao wamekuwa wakichumbiana kwa kipindi cha takriban miaka miwili walivishana pete mbele ya wanafamilia na marafiki wachache .

Katika video iliyochapishwa Instagram na mmoja wa marafiki zao, mwanamuziki Timeless Noel, Bi Musila alionekana akionekana akiongozwa na mwanawe mkubwa  hadi kwa mume wake Guardian Angel .

Musila alitembea kwa mwendo wa aste aste hadi pahali mpenzi wake alikuwa amemsubiri huku muziki aina ya Jazz ukicheza.

Guardian Angel kwa wakati huo alionekana kuwezwa na hisia na kutirirkwa na machozi ya furaha. Mwanamume aliyekuwa amemsimamia alionekana akimsaidia na kitambaa cha kufutia machozi.

Ilikuwa siku maalum kweli kwa familia ya Omwaka kwani pia walisherehekea siku yake ya kuzaliwa anapohitimu miaka 33.

Wanamitandao wameendelea kuwasherehekea wapenzi hayo kwa hatua kubwa ya maisha ambayo walipiga.

@blessednjugush Kheri njema, Hongera

@timelessnoel najivunia kuwa emcee.. Hongera ndugu

@kambuamuziki Anayepata mke

@magreatmumbi Mapenzi tight kama kifuniko ya gas.. walisema mtaachana lakini watangoja sana.. eeh

@dkkwenyebeat Hongera

@mojishortnbabaa Hongera