YY asema wanawake hawajui njia ya kutongoza wanaume

Muhtasari

•YY alichapisha kanda ya video ambayo  alikuwa akitoa maelezo kuhusu walivyo wanawake wa humu nchini

•Alieleza si lazima mwanamme ndiye   mwazilishi wa mahusiano kama inavyofikirika, ila pia mwanamke anaweza kuwa na ujasiri  wa kukatia mwanamme anayetamani  na angetaka kuazisha mahusiano naye

yy
yy

Mchekeshaji wa Churchill Show, Oliver Otieno almaarufu  YY siku ya Jumanne alisema wanawake wa humu nchini  hawajui kupenda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ,Jumanne alichapisha kanda ya video ambayo  alikuwa akitoa maelezo kuhusu walivyo wanawake wa humu nchini, alieleza si lazima mwanamme ndiye   mwazilishi wa mahusiano kama inavyofikirika, ila pia mwanamke anaweza kuwa na ujasiri  wa kukatia mwanamme anayetamani  na angetaka kuazisha mahusiano naye

"Baada ya miaka mingi ya uzoefu na utafiti wangu hatimaye nimehitimisha kuwa..... wanawake hawajui namna  kutongoza wanaume. Ushawai gundua 99% ya wanawake walio jaribu kutongoza mwanamme huwa haifaulu,, unajaribu,.. unafanya kila kitu aingii. umeshindwa kabisa...alafu unafikiria umekataliwa... mmmh apana vyenye unafanya ndio shinda. "

Aliendelea kukiri wanawake huwa hawajui kuonyesha mahaba  kwa wanaume, na hio usababisha mwanamme kukataa kuamini kama anapendwa kikweli.

"hamnanga saa ya mapenzi, hamnanga ata unaendelea aje? kuna huu mradi niliona ulizindua hivi majuzi unafanya vizuri. pongezi ....tumia maneno kama hizo...anzia mbali kwanza.

Isitoshe aliwaonya na hii tabia ya kuruka hatua zingine kwenye mahusiano huku akisema pia wao wakitongozwa  hivo hawawezi kubali mahusiano yoyote

 

"hii yenu ati huko na mke,umeoa,nataka kuwa mke, uko na watoto, nataka kuwa mama wa watoto wako... ata salamu hakuna, hakunanga ata unaendelea aje aaah... ata nyinyi mkikatiwa hvo huwa hamukubali wanaume " alisema YY