Huddah Monroe awapa onyo kali marafiki ambao hawaungi mkono biashara yake

HUddah Monroe
Image: maktaba

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara maarufu humu nchini Alhuda Njoroge almaarufu Huddah Monroe  amefunguka wazi na kusema ni jambo la kushangaza kuona marafiki wengi aghalabu ndio huwa wanakosa kununua bidhaa ambazo mtu anauza.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Huddah ameeleza kero kwamba wanaojiita watu wa familia na wale marafiki zake hawapendi kumsaidia kwa kuendeleza biashara yake 

"Kitu cha kuchekesha ni kwamba watu wanaonunua bidhaa zangu sio marafiki au familia yangu. Marafiki wawili au watatu ndio tu hufanya hivyo " Alisema

Alisema wanaomuunga mkono kwa kiwango kikubwa ni watu ambao hawajuani na ambao si marafiki zake huku akieleza kazi ya marafiki nikumuomba vitu bila malipo.

"Ni wageni wanaoniunga mkono. Marafiki zangu daima huomba vitu vya bure na huwa hawataki niseme" Alisema Huddah

Kutokana na tabia hio ya omba omba  mrembo huyo amewaonya kwamba wasisikie vibaya endapo akakatiza mazungumzo nao.

"Ikiwa haununui bidhaa zangu, ninakukata" Huddah aliwambia marafiki zake

mrembo huyo tajiri ambaye amekuwa Dubai karibu miaka miwili, alisema kwamba msaada wake mwingi hutoka kwa watu wasiowajua na sio marafiki na familia yake. ,” Huddah alichapisha.