"Zaa wako unyoe!" Vera Sidika aapa kutopitisha wembe kichwani mwa bintiye kamwe

Muhtasari

•Vera ambaye anajulikana kutowapa nafasi wakosoaji amewaarifu wale ambao hawaridhishwi na jinsi anavyotunza nywele ya bintiye wamkome na waangazie watoto wao wenyewe.

•Amewaomba wale  wanaomwambia aache kujigamba na nywele ya kwanza ya bintiye wamkome kwani hana mpango wowote wa kubadilisha mawazo yake wakati wowote kutoka sasa.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amewajibu baadhi ya wanamitandao ambao wamekuwa wakimshinikiza anyoe kichwa cha binti yake Asia Brown,

Kupitia mtandao wa Instagram, kikundi kikubwa cha wanamitandao kimekuwa kikimkosoa mama huyo wa mtoto mmoja kwa kuachilia nywele ambayo binti yake alizaliwa nayo iendelee kumea huku wengine wakimweleza itabadilika pindi tu atakapomnyoa.

Vera ambaye anajulikana kutowapa nafasi wakosoaji amewaarifu wale ambao hawaridhishwi na jinsi anavyotunza nywele ya bintiye  ya 'Kiarabu' wamkome na waangazie watoto wao wenyewe.

"Zaa wako unyoeee!! Kama uko naye basi muangalie yeye. Usiniambie jinsi nitalea mtoto wangu!" Vera aliwajibu wanamitandao waliomwomba anyoe bintiye.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 ameapa kwamba kamwe hatawahi kukaa nywele ya binti yake.

Amewaomba wale  wanaomwambia aache kujigamba na nywele ya kwanza ya mtoto huyo mwenye umri wa miezi miwili kwa sasa wamkome kwani hana mpango wowote wa kubadilisha mawazo yake wakati wowote kutoka sasa.

"Afadhali mkome kuniambia  'ngoja hadi unyoe nywele kwanza na uone jinsi itakavyoonekana' Hapana. Sitamkata nywele kamwe. Hilo nimeamua!! Nyinyi nyote endelea na kukata nywele za watoto wako. Nikose hapo" Vera alisema.

Mwanasoshalaiti huyo alifichua sura ya bintiye kwa mara ya kwanza mnamo Desemba 20 na amekuwa akionyesha ulimwengu wote urembo wake kila uchao tangu siku hiyo.