'Aliniacha baada ya kupata vyombo chafu jikoni,'Mwanamume asimulia masaibu ya ndoa yake

Muhtasari
  • Wengi hupitia na kupigania ndoa yao, lakini wengi wao huchoka na kuwaacha wapenzi wao, huku wakiendelea na maisha yao
sad man
sad man

Je sababu yako kuu ya kugura au kumuacha mke wako au kuachwa na mke wako kwenye ndoa yako ni ipi?

Wengi hupitia na kupigania ndoa yao, lakini wengi wao huchoka na kuwaacha wapenzi wao, huku wakiendelea na maisha yao.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii jamaa mmoja aliwaacha wengi midomo wazi baada ya kufichua sababu kuu ambayo ilimfanya mke wake amuache.

"Mke wangu aliniacha mwezi wa Desemba mwaka jana baada ya kutoka sherehe na kupata kwamba sijaosha vyombo alikusanya virago vyake na kuenda kwao

Ilhali ata baada ya kuniambia ameenda kwao niliambiwa kwamba hajafika nyumbani, na ameniachia watoto 2, wiki jana alinipigia simu na kuniambia kwamba anataka kurudi tena, sijui nimwwambie nini kwani mwanamke kama huyu siwezi kuvumilia maisha naye, nimekuwa nikifanya mambo mengi na kuvumilia mengi lakini sasa amenifika kwenye koo, nahitaji ushauri kutoka kwa wanamitandao."