'Hapana cheza na Bughaaa,'KRG The Don asherehekea kusitishwa kwa akaunti yake Edgar Obare

Muhtasari
  • KRG The Don asherehekea kusitishwa kwa akaunti yake Edgar Obare
KRG
Image: Hisani

Msanii KRG The Don amedai kwamba ndiye amesababisha akaunti yake mwanablogu Edgar Obare kusitishwa.

Mnamo Januari 7 Edgar kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliwatangazia mashabiki wake kwamba akaunti yake ya instagram ya BNN imefutwa.

Anajulikana sana kwa chaneli yake ya YouTube, BNN, inayowakilisha Bandana News Network.

Muda mfupi uliopita, akaunti yake kuu ya Instagram ilipotea baada ya kuwafichua watu mashuhuri kwa madai ya kuhusika na ulaghai wa pesa.

Muda mfupi baadaye, KRG the don alijitokeza akijipiga kifua na kujipongeza kwa kuwajibika kwa kufuta akaunti.

Kwa hiyo, maneno yake ni ya kweli kadiri gani? Anaweza kuwa tu anatafua kiki? Maneno yake yaliwafanya baadhi ya mashabiki kumtusi.

"Ediga kibare Hapana Cheza na Bughaaa ….. sayari hii ni salama bila  BNNKE….. wanafunzi wake wanaweza kulia kwenye sekta ya maoni

Nilisema kwamba nitafuta BNNKE kwa hii sayari wakafikiria ni mzaha nani anacheka sasa," Aliandika KRG.

KRG The Don ni msanii wa muziki kutoka Kenya aliyeorodheshwa miongoni mwa wasanii wachanga matajiri zaidi nchini.

Akiwa na umri mdogo, anajieleza kuwa bilionea wa Kenya asiye wastani. Licha ya madai na uvumi kuwa utajiri wake unatokana na biashara haramu aka utakatishaji fedha, KRG The Don amekanusha hayo na kusema yuko tayari kuhesabu pesa zake.