Kuonewa tu!Sababu iliyofanya akaunti ya Instagram ya Edgar Obare kufutwa

Muhtasari
  • Sababu iliyofanya akaunti ya Instagram ya Edgar Obare kufutwa
Edger Obare
Edger Obare
Image: Hisani

Hii sio mara ya kwanza akaunti yake Edgar Obare kufutwa au kusitishwa, kwani mwaka jana akaunti yake ilifutwa baada ya kufichua siri ambazo zimekuwa katika kikundi cha 'wash wash'.

Siku ya Ijumaa wakenya waliamkia habari kwamba akaunti yake ya instagram iliyokuwa inafahamika kama BNN imefutwa, huku wengi wakiulizana sababu kuu ya kusababisha kisa kama hicho.

Edgar kupitia kwenye akaunti nyingine inayo fahamika kama Uncle Edgar alifichua sababu ya akaunti yake ya ya awali kufutwa.

"Hii ni akaunti yangu mpya ya Instagram. Wacha tuanze tena pamoja, sio kwenda juu. Tunabadilika tu na kuendelea," aliandika.

Pia alidai kwamba ufichuzi' aliotoa dhidi ya mtangazaji wa Kiss100 Fm, Kamene Goro, ndio sababu Instagram ilitaja kuzima ukurasa wake.

"Hii ndiyo hadithi iliyolemaza akaunti yangu. Walitaja kwamba nilienda kinyume na miongozo ya jamii-unyanyasaji. Kuonewa tu," mwanablogu huyo alisema.

Saa chache baada ya kutangaza kusitishwa kwa akaunti yake msanii KRG The Don alisherehekea habari hizo, huku akidai kwamba ndiye aliyesababisha hayo.