logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kajala Masanja afurahia mazoezi ya Peter Msechu

Kulingana naye alisema Kajara amekuwa akitaka kujua siri ya kupunguza ukubwa, na hivyo akamuomba aweze kumsaidia kupunguza ukubwa wa mwili wake

image
na Radio Jambo

Yanayojiri10 January 2022 - 10:16

Muhtasari


•Dada yangu kajala ..Amenisumbua sana kwa muda wa karibia mwaka mzima ananiuliza kaka unafanyaje kupungua nikawa namwambia siri ni mazoezi na lishe bora

•Amefurahi sana kukutana na mimi na amefurahia mazoezi niliyompa. nina imani atapungua sasa na kufikia mwili wa ndoto yake

Peter Msechu

Mwanamuziki wa  Bongo Peter Msechu siku za hivi karibuni ameonekana na mwanamtindo  Kajala Masanja huku akidai mazoezi aliyompa Kajala ameyapenda.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Msechu  amewajibu mashabiki ambao wamekuwa wakitaka kujua kinachoendelea  baina yake na Kajara. 

Kulingana naye alisema Kajara amekuwa akitaka kujua siri ya kupunguza ukubwa, na hivyo akamuomba aweze kumsaidia kupunguza uzani wake 

"Dada yangu kajala ..Amenisumbua sana kwa muda wa karibu mwaka mzima ananiuliza kaka unafanyaje kupungua nikawa namwambia siri ni mazoezi na lishe bora akaniambia naomba unisaidie na mimi kwenye mazoezi nipungue nikawa busy sana sana sikupata muda kabisa." alisema Msechu

Vile vile. alidokeza kilichomfanya ajitolee mwaka huu  kumpeleka  Kajala kumfundisha  mazoezi.

"Akawa  ananipigia simu analia sana hadi makamasi yanamshuka anasema kaka unanionea, yaani kunipa dakika  kadhaa tu unifundishe mazoezi yako, unashindwa. nikawa namwambia Kajala tulia usilie jamani futa makamasi akawa ananyamaza basi mwaka huu ndio nikasema nimuonee huruma walau leo nimpe mazoezi hapa @adreline255 kidogo."

Isitoshe alieleza baada ya kumpeleka kwenye mafunzo hayo, Kajara akuweza kuficha furaha aliyokuwa nayo huku akimwahidi atapungua na kufikia mwili wa ndoto yake

"hivyo leo amefurahi sana kukutana na mimi na amefurahia mazoezi niliyompa. nina imani atapungua sasa na kufikia mwili wa ndoto yake"


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved