Konde Gang ya Harmonize yamwachilia Country Boy

Muhtasari

•Mkataba Kati Ya Konde Music Worldwide Na @countrywizzy-tz Umemalizika Hii Leo Tar 8 January 2022

Harmonize na Country Boy
Harmonize na Country Boy
Image: hisani

Msimamizi wa lebo ya Konde Gang msanii Harmonize ametangaza kusitisha uhusiano wa kazi na msanii Country Boy.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Konde Gang ilitoa taarifa kwamba wamekubaliana kuacha kufanya kazi na rapa huyo baada ya kumalizika kwa mkataba wa mwanamuziki  huyo ambaye aikuwa amesaini mkataba na lebo hio.

Kwenye taarifa hio walisema kuanzia tarehe 8 januari mwaka huu, Country Boy atakuwa msanii atakayekuwa anajisimamia binafsi kwa kazi za muziki wake. 

"Mkataba Kati Ya Konde Music Worldwide Na @countrywizzy-tz Umemalizika Hii Leo Tar 8 January 2022.Kuanzia Leo Country Wizzy Atakuwa Msanii anaejitegemea Baada Ya Kuafikia Makubaliano Ya Pande Zote Mbili.

Isitoshe, walimtakia mwanamuziki huyo kheri njema katika safari yake ya muziki.

"Konde Music Worldwide Inamtakia Kila Lenye Kheri Country Wizzy Kwenye Career Yake Ya Music Pamoja Na Maisha Kwa Ujumla"