Mulamwah bado anamiliki akaunti ya binti yangu-Carol Sonie afunguka kuhusu usimamizi wa akaunti ya binti yake

Muhtasari
  • Miezi kadhaa iliyopita, Mulamwah na mkewe carol Sonie walitengana baada ya kumkaribisha binti yao mzaliwa wa kwanza
  • Watu wengi walibaki wakijiuliza ni nini chanzo cha talaka hiyo lakini yote yaliambulia patupu
Image: INSTAGRAM// CAROL SONNIE

Aliyekuwa mpenzi wake chekeshaji Mulamwah,Carol Sonie kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu anayemiliki akuanti ya mitandao ya kijamii ya binti yake.

Miezi kadhaa iliyopita, Mulamwah na mkewe carol Sonie walitengana baada ya kumkaribisha binti yao mzaliwa wa kwanza.

Watu wengi walibaki wakijiuliza ni nini chanzo cha talaka hiyo lakini yote yaliambulia patupu.

Mulamwah alifunguka akisema kuwa baadhi ya mambo ni bora yaachwe bila kusemwa badala ya kusema ni nini chanzo cha talaka na kumuumiza mke wake wa zamani.

Saa kadhaa zilizopita, Carol alichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram akiwapa wafuasi wake fursa ya kumuuliza swali lolote ambalo wamewahi kutaka kumuuliza.

Mmoja wa wafuasi wake alimuuliza ni nani anayemiliki na kusimamia akaunti ya binti yao ya Facebook kwa vile ingali hai hata baada ya wao kutalikiana.

Carol alijibu akisema kuwa Baba wa bintiye, Mulamwah ndiye anayemiliki na anaidhibiti na hana tatizo na hilo.