Nyota wa 'Full House' Bob Saget apatikana amefariki

Muhtasari

• Bob Saget mcheshi wa Marekani ambaye atakumbukwa kwa mtindo wake wa kufurahisha mamilioni ya watu  kwenye kipindi cha televisheni cha 'Full House' katika miaka ya 1980 na 1990.

Bb Sajet
Bb Sajet
Image: hisani

Mcheshi wa Marekani na nyota wa 'Full House' Bob Saget alipatikana amefariki kwenye chumba kimoja cha Florida, Jumapili baada kutumbuiza mashabiki wake kwenye onyesho la  PV_ConcertHall huko Jacksonville.

Bob Saget mcheshi wa Marekani ambaye atakumbukwa kwa mtindo wake wa kufurahisha mamilioni ya watu  kwenye kipindi cha televisheni cha 'Full House' katika miaka ya 1980 na 1990.

Siku ya Jumamosi usiku,  kupitia  ukurusa wake wa twitter, mcheshi  huyo alikuwa akiburudisha mashabiki wake, katika ukumbi wa tamasha wa Ponte Vedra, ambapo aliandika kwenye ukurasa wake kwamba  alipenda onyesho alilofanya usiku huo.

" Nilipenda onyesho la usiku wa leo @PV_ConcertHall huko Jacksonville. Watazamaji wenye shukrani. Asante tena kwa @RealTimWilkins kwa kufungua. Sikujua nilifanya seti ya saa 2 usiku wa leo. Nimevutiwa tena na uraibu huu wa furaha." aliandika  Bob Saget.

Saget amefariki akiwa na umri wa miaka 65, na kiini cha kifo chake bado hakijabainika japo uchunguzi unaendelea kufanywa kubainisha kilichosababisha kifo chake.

Jumapili  familia yake ilisema "Tumesikitishwa sana kuthibitisha kwamba mpendwa wetu Bob amefariki leo"

Mbali na umaarufu wake wa 'Full House' Saget pia atakumbukwa kama shabiki maarufu wa "America's Funniest Home Video," ambapo alihudumu kama mtangazaji kutoka mwaka 1989 hadi 1997 

Katika taarifa iliyochapishwa na jarida la People Daily ilisema familia ya Saget inaomboleza  kumpoteza.

"Alikuwa kila kitu kwetu na tunataka mjue ni kiasi gani aliwapenda mashabiki wake, akiwatumbuiza moja kwa moja na kuwaleta  pamoja watu wa tabaka zote kwa kicheko."