Kambua asimulia unyanyapaa aliopitia baada ya kumpoteza mtoto

Muhtasari

• Kupoteza mtoto ni mwiko. Nimejifunza hili kutoka kwa ninaowapenda ambao wametembea safari hii .

• Unyanyapaa, aibu, kukosolewa, hukumu, maswali yasiyo na mwisho na ushauri usio na mwisho yote ni mambo aliyokumbana nayo.

Mwanamuziki Kambua
Mwanamuziki Kambua
Image: Hisani

Msanii wa nyimbo za injili Kambua Jumatatu alifunguka kuhusu mambo aliyoyapitia alipoteza mtoto wake wa pili.

Kambua alitumia  ukurusa wake wa Instragram kueleza aliyokumbana nayo wakati alipokuwa akiomboleza  mtoto huyo wake. 

Alisema amekuwa akisoma kitabu ambacho kilikuwa kikiangazia masuala mbalimbali kuhusiana na huzuni iliyojadiliwa na pia kupeana mafunzo kadha kwa kadha.

 Mama huyo wa watoto wawili, anasema kupoteza mtoto hakuathiri mzazi pekee ila  pia familia nzima kwa jumla.

"Kupoteza mtoto hakuathiri mzazi pekee, pia kunaathiri ndugu, babu, bibi, shangazi, marafiki na kila mtu ambaye alikuwa na matumaini ya kukutana na mtoto."  alisema Kambua.

Aliongeza kwamba kupoteza mtoto katka baadhi ya jamii huchukuliwa kama mwiko, huku akikiri aliyopitia kipindi hicho cha kuomboleza mtoto wake.

"Kupoteza mtoto ni mwiko. Nimejifunza hili kupitia watu ninaowapenda ambao wametembea safari hii . Unyanyapaa, aibu, kukosolewa, hukumu, maswali yasiyo na mwisho na ushauri usio na mwisho . Lakini nimejifunza kulinda imani yangu kwa ukali na kwa gharama" yo yoyote ile.”