Mcheshi Mulamwah amejitokeza hadharani kuzungumzia kutengana kwake na mama wa mtoto wake Carrol Sonie.
Mulamwah alikuwa akizungumza na kituo kimoja cha radio nchini, alieleza sababu zilizofanya kuachana na mpenzi wake wa zamani na kusema kuwa waliachana wakati Sonie alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu, lakini alichagua kukaa kimya hadi pale mtoto alipozaliwa.
Aliongeza kwamba mpenzi huyo wake wa zamani hakuwa mvumilivu, kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo kuweza kukidhi baadhi ya matakwa yake ila alianza kuomba usaidizi kwa watu wengine.
"Ningeomba sana hata kwa mahusiano yake ingine aendelee kuwa mtulivu na mvumilivu...hizi vitu zote tutapata. unapata labda kuna wakati singeweza kukimu hiki na kile. yeye angeenda kutafuta mahali fulani ama kwa jamaa wake na nilikuwa nakwazika kweli kweli," Mulamwah alisema aliyokuwa akipitia kipindi hicho walichokuwa na Sonie.
Isitoshe hakusahau kuwashauri warembo, "Ningependa kuambia madem watupatie wakati, usiharakishe, utapata hayo matunda yanaendea mwengine,"