Hamisa Mobeta atangaza kuzuru Kayole, Kenya

Muhtasari

• Hamisa ametoa taarifa kuwa siku ya Jumamosi atakuwa nchini Kenya kuchangisha pesa ambazo zitasaidia mayatima kufadhili masomo yao.

• Zimesalia siku chache tu kufikia tarehe 15 Januari. Tafadhali Changia unachoweza.

Hamisa Mobeto
Hamisa Mobeto
Image: Instagram/Hamisa

Mwanasosholaiti  Hamisa Mobeto ametangaza mpango wa kuzuru kenya kusaidia kituo cha watoto yatima cha Kayole  kuchangisha pesa kwa ajili ya mahitaji ya watoto hao.

Kupitia ukurusa wake wa Twitter Hamisa, ametoa taarifa kuwa siku ya Jumamosi atakuwa nchini Kenya kwa ajili ya kuchangisha pesa ambazo zitasaidia watoto hao kwa lengo la kufadhili elimu yao.

Aidha aliwaomba watu  wahisani kujitokeza ili kufanikisha mchango huo. 

"Habari za asubuhi, watu wangu wa Kenya; zimesalia siku chache tu kufikia tarehe 15 Januari. Tafadhali Changia unachoweza ili Kusaidia. Tunajaribu kuwasaidia watoto wetu huko Kayole ili warudi shule."

Aliwaeleza wafuasi wake  wakutane Bread Gate Shujaa Mall saa nane  kwa hafla hio kubwa ya kuchangisha fedha.

"Tukutane Bread Gate Shujaa Mall saa 2 usiku kwa Hafla ya kuchangisha fedha." alisema Hamisa

Hamisa ambaye ni  mama mtoto wa Diamond, hivi majuzi ameonekana kuzuru maeneo mbali mbali na mwanamziki wa Marekani Rick Ross amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi.