Edday Samidoh apendekeza Julie Mbogo kuwa seneta wa Nairobi

Muhtasari

• Edday alitangaza anapendekeza  rafiki  yake wa miaka mingi Julie Mbogo kuwania kiti cha useneta  wa Nairobi  kuliko  Mama wa mtoto wa Samidoh, Karen Nyamu.

Samidoh na mkewe Edday
Samidoh na mkewe Edday
Image: instagram/edday

Mke  wa staa wa Mugithi almaarufu Samidoh, Edday Nderitu ametangaza hadharani anayependelea kuwa seneta wa Nairobi.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Edday alitangaza anapendekeza  rafiki  yake wa miaka mingi Julie Mbogo kuwania kiti cha useneta  wa Nairobi  kuliko  Mama wa mtoto wa Samidoh, Karen Nyamu.

Edday Samidoh alichapisha picha ya  Julie huku akisema "seneta wangu wa Nairobi"

 

Mashabiki wake wa mtandao hawakufumbia macho ujumbe wake  ambapo walitoa maoni yao  huku wakipongeza kwa kusimama na rafiki yake. Baadhi ya maoni yao yalikuwa kama ifuatavyo; 

@susankarimi7 Una haki ya kumuunga  utakaye. kama kuna mtu hajafurahishwa na hilo aende akaposti  mwenye anamuunga kwa ukurasa wake alaa..

@musyoka_musau_ Huyu hawezani na force ya Nyamu wacha aibu ndogo...

@wambomacharia-Jamani! Nampenda Edith ndo huyu seneta wetu kanairo. Huko ukienda nakufuata ooh

Mke wa samidoh aidhinisha BFF kwa kiti sawa na Karen Nyamu.