Jason Momoa atangaza rasmi kuachana na mkewe Lisa Bonet

Muhtasari

•Jason Momoa ametangaza kuachana na mpenzi wake Lisa Bonet baada  ya kuafikiana na mkewe kuachana.

•Wapenzi hao wawili walihudumu kwenye ndoa kwa takriban miaka mitano ambapo walifanikiwa kupata watoto wawili

 

Jason Momoa
Jason Momoa
Image: instagram/ Jm

Muigizaji wa kimataifa Jason Momoa ametangaza kuachana na mpenzi wake Lisa Bonet baada  ya kuafikiana makubaliano kuachana.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Jason alieleza kuwa wametalikiana na mkewe Lisa Bonet.

Wapenzi hao wawili walikuwa katika ndoa kwa takriban miaka mitano ambapo walifanikiwa kupata watoto wawili.

 Jason na Bonet walitoa ujumbe kwamba  kutokana na mashabiki wao ambao wamamekuwa wakiwapa motisha kila wakati, wameamua kutangaza rasmi kuvunjika kwa ndoa yao.

"Sote tumehisi msukumo wa na mabadiliko ya nyakati hizi ... mapinduzi yanatokea na familia yetu haijasazwa...kuhisi na kukua kutokana na mabadiliko ya mitetemeko katika ndoa. Na hivyo  kwa pamoja tunatoa taarifa kwamba kunatengana ." alisema Jason na Bonet

vile vile  walitoa sababu za kuamua kutangaza kuvunjika kwa ndoa yao.