Niko tayari kumzalia Bahati mtoto mwingine Diana B asema

Muhtasari

• Diana B amejitokeza wazi na kumwambia mumewe,Bahati yuko tayari kumzalia mtoto mwingine.

Bahati na mkewe Diana Marua
Bahati na mkewe Diana Marua
Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Mwanamuziki Diana Marua almaarufu Diana B amejitokeza wazi wazi na kumwambia mumewe, Bahati kwamba yuko tayari kumzalia mtoto mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana aliwaambia mashabiki wake kuwa yuko tayari  kupata mimba tena.

Wapenzi hao Diana na Bahati, hivi majuzi wamewajibu wakosoaji wao kuwa watakaa pamoja hadi kifo kiwatenganishe.

Diana amekuwa kwenye ndoa kwa miaka sita na kuweza kubarikiwa na watoto wawili ambao ni Heaven na Majesty.

Rapa huyo alibainisha kuwa anataka kupata mtoto mwingine na kipenzi chake mwaka huu, kulingana naye mayai yake yalikuwa yanacheza, na kumshawishi apate mtoto mwingine.

“Leo usiku itabidi bahati @bahatikenya acheze kama yeye!!! Mwaka huu, nampa mtoto mwingine, mmoja wa mwisho” Alisema Diana.

Diana na Bahati wanajivunia familia yao kwani kila mara huonyesha watoto wao kwenye mitandao ya kijamii.