"Sasa nini imekuua?" Akothee aomboleza mfanyikazi wake aliyefariki ghafla

Muhtasari

•Rais huyo wa kina mama wasio na waume wa kujitangaza amebaki akishangaa bustani yake na mbwa wake na familia ya marehemu zitachungwa na nani kufuatia msiba huo.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali maashuri Esther Akoth almaarufu kama Akothee yuko katika hali ya kuomboleza kufuatia kifo cha ghafla cha mfanyikazi wake mmoja.

Mama huyo wa watoto watano amempoteza mfanyikazi wake ambaye kwa kawaida alihudumia bustani yake na mbwa wake.

Kifo cha mfanyikazi huyo kimempata mwanamuziki huyo kwa mshtuko mkubwa na kumuacha na maswali chungu nzima yasiyojibika.

Rais huyo wa kina mama wasio na waume wa kujitangaza amebaki akishangaa bustani yake na mbwa wake na familia ya marehemu zitachungwa na nani kufuatia msiba huo.

"Kifo cha ghafla cha mfanyakazi wangu mmoja kimeniacha nikijiuliza, inakuwaje mtu aamke akiwa amekufa? Charo sasa nini imekuuaa? Na hii garden umeachia nani wewe? na akina salome? Bibi yako na watoto umeachia nani Charo? Charoooooooo! Charoo jina rahisi katika kinywa changu" Akothee ameomboleza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Wanamitandao wameendelea kumfariji mwanamuziki huyo na kumtakia mfanyikazi huyo wake mapumziko ya amani.