Kuna siku kila kitu kitakuwa sawa,'Ushauri wa Mbosso kwa mashabiki

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za bongo na ambaye amesajiliwa katika lebo ya muziki ya Wasafi Mbosso kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri mashabiki wake jinsi ya kumshukuru Mungu
66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n
66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n

Msanii wa nyimbo za bongo na ambaye amesajiliwa katika lebo ya muziki ya Wasafi Mbosso kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri mashabiki wake jinsi ya kumshukuru Mungu.

Pia msanii huyo amesema kwamba wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kile wanamiliki kwani kuna baadhi ya watu ambao hawana chochote ila wanaamini kwamba kuna siku Mambo yatakuwa sawa.

Mbosso anafahamika sana kupitia kwa nyimbo zake ambazo zimepokelewa vyema na mashabiki mitandaoni.

"Unaweza kuwa hijafaniiwa sana katika maisha yako,au pengine hujatimiza ndoto yako ila niamini maisha unayoishi ni ya daraja la juu sana kama ukilinganisha na walio chini yako," Alisema Mbosso.

Aliendela na ujumbe wake na kusema kuwa;

"Mshukuru sana mwenyezi Mungu,kidogo chako ulichonacho wewe kuan watu hawana kabisa na hawajachoka kumuomba Mungu na kumshukuru Mungu na wanaamini kuwa kuna siku kila kitu kiakuwa sawa

Tusiache kumuomba na kumshukuru Mungu."