Hamisa Mobeto, Tanasha Donna wabarizi pamoja kudhihirisha urafikia wao

Muhtasari

•Tanasha Donna na Hamisa Mobeto  Jumapili walitumia wakati wao mwingi pamoja huku ikibanika wamekuwa marafiki wakubwa siku za hivi za karibuni.

Tanasha Donna na Hamisa Mobeto
Tanasha Donna na Hamisa Mobeto
Image: Hisani

Wapenzi wa zamani wa msanii sifika kutoka nchini Tanzania Diamond Platinumz, Tanasha Donna na Hamisa Mobetto walidhihirisha urafiki wao kwa mashabiki huku wakichapisha picha kadhaa kuonyesha ukaribu uliopo kati yao.

Siku ya Jumapili wawili hao walitumia wakati wao mwingi pamoja huku na kudhibitisha kuwa wamekuwa marafiki wakubwa siku za hivi za karibuni.

Malkia hao wawili ambao ni mama wa watoto wa Diamond  wamekuwa wakidhirisha  urafiki huo kwenye  mitandao ya kijamii

Alhamisi wakati Hamisa Mobeto alitangaza  rasmi kuwa atakuwa anazuru nchi ya  Kenya,Tanasha  hakuficha uchu wa kutaka msanii huyo kumtemtembelea kwake hata kama ni kwa muda tu.

Kwa mujibu wa mfululizo wa picha zinazoonekana kwenye ukurasa  wao wa Instagram, wawili hao walionekana  wakiwa wanabarizi pamoja katika chumba cha kifahari huku wakionekana wenye furaha kubwa.

Urafiki kati ya  Tanasha na Hamisa uliimarika zaidi wakati Tanasha alimhusisha Hamisa kwenye video moja akiwa na masauti.