Hongera!Milly Wajesus na Kabi Wajesus watarajia mtoto wao wa pili

Muhtasari
  • Milly Wajesus na Kabi Wajesus watarajia mtoto wao wa pili
Image: Milly Wajesus/Instagram

Wanabiashara na wauanda maudhui Milly Wajesus na Kabi Wajesus, wamepata wafuasi wengi mitandaoni kutokana na video zao wanazopakia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na kwenye mtandao wa Youtube.

Licha ya changammoto abazo wawili hao wamekuwa wakikumbana nazo kwenye ndoa yao, wamewahakikishia mashabiki wao kwamba ndoa ni kitu muhimu maishan.

Siku ya JUmanne wawili hao waliwatangazia mashabiki wao kwamba wanatarajia mtoto wao wa pili.

Kupitia kwenye ukurasa wa Milly wa Instagram alimshukuru MUngu kwa kumpa nafasi nyingine ya kuwa mzazi.

"Tunayo furaha kubwa hatimaye kushiriki habari za kusisimua na familia yetu mtandaoni. FAMILIA YA WAJESUS INAENDELEA NA TUNAMPA MUNGU UTUKUFU WOTE. Ametuchagua kuwa wazazi kwa mara nyingine tena na kuunganisha pamoja mdogo ili kujiunga na familia yetu.

Kwa @kabiwajesus sikuwahi kufikiria njia bora zaidi ya kushiriki baraka zetu na familia yetu ya mtandaoni,"Milly na Kabi Waliandika.

Tunawatakia kila la Kheri katika safari yao.