Sailors Gang yakanusha madai ya Rachel Mwalimu aliyayosema

Muhtasari

•Sailors  Gang ilitambulika kuwa mojawapo ya wanzilishi  wa mtindo wa aina ya muziki wa Gengetone ambao ulipendwa sana hasa na vijana wa kizazi kipya.

•Mwalimu Rachel alikuwa meneja wao ambaye alikuwa anaendesha shughuli zao vizuri  hadi siku ile waligundua kiasi  cha pesa alichokuwa akipata dhidi ya kiasi walichokuwa wakipokea.

Sailors-3-551x600
Sailors-3-551x600
Image: Hisani

Mmoja wa kikundi cha sailors gang Lexxy Yung amejitokeza na kupinga kauli ya muigizaji Mwalimu Rachel ambayo alisema si yeye alikuwa chanzo kuu cha kundi hilo kusambaratika.

Sailors  Gang ilitambulika kuwa mojawapo ya wanzilishi  wa mtindo wa aina ya muziki wa Gengetone ambao ulipendwa sana hasa na vijana wa kizazi kipya.

Kupitia ukurusa wa Instagram, Lexxy Yung amekanusha madai ambayo mwigizaji Mwalimu Rachael alisema hivi majuzi kufuatia kile alichoeleza kuwa yeye aliwasaidia kukuza muziki wao na kufanya wajulikane zaidi humu nchini.

Kulingana naye Mwalimu Rachel alikuwa meneja wao ambaye alikuwa anaendesha shughuli zao vizuri  hadi siku ile waligundua kiasi  cha pesa alichokuwa akipata dhidi ya kiasi walichokuwa wakipokea.

"Ninataka watu wajue ukweli wa  kilichokuwa kikiendelea baina yetu na Mwalimu..Mwalimu hatukuwa na muktaba na yeye... ilikuwa tu urafiki. tukamuagiza atusimamie kama Meneja na kweli bila yeye hatungejulikana...lakini yeye kuchukua akaunti zetu  haikuwa jambo nzuri ..alichukua Mdudo,Boomplay,  akachukua skiza, Youtube , twitter na Istagram  na hakutaka kurejesha" alieleza Yung.